Papa Francis adai hana wazo la kujiuzulu

14Mar 2024
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Papa Francis adai hana wazo la kujiuzulu

​​​​​​​KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amedai kuwa hana nia ya kujiuzulu kwani anahisi afya yake ni nzuri na anaweza kuendelea na majukumu yake.

​​​​​​​KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

DW imeripoti kuwa, Papa Francis ameyasema haya katika kitabu kipya ambacho dondoo zake zimechapishwa katika gazeti la Corriere della Sera huko Nchini Italia.

Katika kitabu hicho kinachotarajiwa kutolewa rasmi Machi 19, Papa anasema wazo la kujiuzulu ni ndoto kwakuwa hana sababu yoyote ya kumpelekea kufanya hivyo.

Francis mwenye umri wa miaka 87 katika miaka ya hivi karibuni ameripotiwa kuugua mara kadhaa, ambapo amekuwa akitumia kiti cha magurudumu au mkongojo kutembea, amekuwa akiugua mafua mara kwa mara jambo lililompelekea kupunguza maongezi yake mbele ya umma.