Mtoto wa Mbowe apigwa butwaa kubadikwa tangazo kuuzwa nyumba yake

28Feb 2024
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mtoto wa Mbowe apigwa butwaa kubadikwa tangazo kuuzwa nyumba yake

DUDLEY Mbowe, ameibua mshangao baada ya kutoridhishwa na Dalali wa Mahakama, Jesca Massawe, kufika nyumbani anakoishi na kubandika tangazo la kupigwa mnada kwa nyumba hiyo, kutokana na deni la Sh. mil 62.7.

Mtoto wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, DUDLEY Mbowe, akibandua tangazo la dalali la kupigwa mnada kwa nyumba hiyo.

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, ilitoa amri ya kupigwa mnada nyumba hiyo na kumteua Jesca Massawe, kutoka Kampuni ya Udalali ya MM Auctioneer &Debt Collectors, kutekeleza amri hiyo.

Tukio hilo limetokea, leo, mkoani Dar es Salaam, Jessica, akiripoti Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mikocheni A, ilipo nyumba hiyo na kisha kubainisha notisi aliyoibandika nyumbani kwa mtoto wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.