Waziri wa ujenzi na uchukuzi, Prof Makame Mbarawa ameambatana na waziri wa fedha Dr. Mwigulu Nchemba mkoani Kigoma kwaajili ya kutembelea miradi ya maedeleo itakayochangia kuufungua mkoa wa Kigoma.
Balozi wa India nchini, Shri Binaya Srikanta Pradhan (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian, Wallace Maugo (watatu kulia), alipotembelea chumba cha habari cha Kampuni ya The Guardian Ltd (TGL) inayochapisha magazeti ya The Guardian na Nipashe, Mikocheni, mkoani Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe na (watatu kushoto) ni Mkurugenzi wa TGL, Joyce Luhanga. PICHA ZOTE: MIRAJI MSALA
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa (wapili kushoto), baada ya kuwasili kwenye ofisi za kampuni ya The Guardian Ltd (TGL) inayochapisha magazeti ya Nipashe na The Guardian, Mikocheni, mkoani Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa TGL, Joyce Luhanga. PICHA ZOTE: MIRAJI MSALA