Balozi wa India nchini, Shri Binaya Srikanta Pradhan (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian, Wallace Maugo (watatu kulia), alipotembelea chumba cha habari cha Kampuni ya The Guardian Ltd (TGL) inayochapisha magazeti ya The Guardian na Nipashe, Mikocheni, mkoani Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe na (watatu kushoto) ni Mkurugenzi wa TGL, Joyce Luhanga. PICHA ZOTE: MIRAJI MSALA Meneja wa kiwanda cha uchapishaji cha TGL, Balasubramaniyan Venkadachalam (kulia), akitoa maelezo kwa Balozi Shri Binaya Srikanta Pradhan (kushoto), kuhusu uchapishaji wa magazeti. Balozi Shri Binaya Srikanta Pradhan (kulia), akimsikiliza Meneja wa EATV na Radio, Lydia Igarabuza alipotembelea studio. Watatu kulia ni Mkurugenzi wa Ubalozi wa India, Santhopsh G R. Balozi Shri Binaya Srikanta Pradhan (wapili kulia), akimsikiliza Mtangazaji wa Redio One, Othuman Suleyman, alipotembelea studio za redio hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile (kulia), akitoa maelezo kwa Balozi Shri Binaya Srikanta Pradhan (wapili kushoto) alipoitembelea kampuni hiyo. Mkurugenzi wa Vipindi wa ITV, Pius Paul (kushoto), akitoa maelezo kwa Balozi Shri Binaya Srikanta Pradhan, jinsi taarifa ya habari inavyorushwa ndani ya studio ya televisheni hiyo.