Kinana: Rais Samia anadhamira ya dhati kufanikisha uchaguzi huru

05Mar 2024
Maulid Mmbaga
Dar es Salaam
Nipashe
Kinana: Rais Samia anadhamira ya dhati kufanikisha uchaguzi huru

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewahakikishia Watanzania kuwa serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kufanya uchaguzi huru na wa haki kuanzia wa serikali za mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Kinana ameyasema hayo leo Machi 5, 2024, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa salamu akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia katika mkutano mkuu wa chama cha ACT -Wazalendo.

 

Amesema wanakwenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani uchaguzi mkuu. Na kwamba kumefanyika mabadiliko ya sheria tatu bungeni, kutokana na maoni mbalimbali ya wadau, ikiwamo Sheria ya vyama vya siasa, tume ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi. 

 

"Nataka niwahakikishie kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia ina dhamira ya dhati katika mwaka huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao kwenye serikali kuu kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki," amesema Kinana.

 

Amesema mbali na kupitisha sheria nzuri ya kuhakikisha kunakuwapo uchaguzi huru na wa haki, pia dhamira ya Rais Samia kufanikisha hilo inajipambanua katika utekelezaji

wake.

Habari Kubwa