NIPASHE JUMAPILI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi maalum kwa Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji (katikati)ikiwa ni ishara ya kutambua jitihada zake katika kufanikisha mpango mpya wa shirika hilo wa kubadili muonekano na taswira yake kijamii na kibiashara hatua ambayo inalenga kuakisi ukuaji wa shirika hilo sambamba maboresho ya huduma zake kwa wateja. Wanaoshuhudia ni Naibu Kamishna wa Bima Tanzania, Khadija Issa Said (Kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya ZIC, Ramadhani Mwalimu Khamis (wa pili kulia) na Balozi wa Bima nchini Wanu Hafidh Ameir (Mb) (kushoto).Hafla ya uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa ZIC ilifanyika jana Zanzibar.