Makonda ameyasema hayo leo Zanzibar, na kueleza kuwa chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Watanzania wameshuhudia haki ikisimamiwa kikamilifu, pamoja na kuhakikisha kila mtanzania anapata haki yake bila kujali rika, elimu kipato, kabila na dini.
“Kwa masikitiko makubwa jana tumepata nafasi ya kumsikia kaka yetu Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA akituhumu na kutoa kauli za kuzalilisha na kufedheesha na kutweza utu wa Kiongozi wetu bila kujali dhamira njema aliyoonyesha Dk. Samia katika ujenzi wa umoja na mshikamano katika taifa letu," amesema.
"Taifa hili kwa mara ya kwanza limeshuhudia haki ikisimamiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na jitihada binafsi za Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais alizozifanya katika kuunda Tume ya Haki Jinai ili kuhakikisha kwamba Mtanzania anapata haki yake,"amesema.
"Mbowe kasema maneno mazito sana, upo wakati tumetafakari ya kwamba hakuna sababu ya kumjibu lakini imefika wakati tukasema hapana... kwanini tumuache apotoshe umma kwa kichecheo ambacho hatuelewi msingi wake ni nini?,” amesema.
"Moja ya hoja kubwa aliyosimama nayo katika mchakato huu wa mswaada wa sheria tatu Sheria ya vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi yenyewe, amediriki kusema hadharani kwamba mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi kilichoundwa na Rais, na mengine kwamba yote yamepuuzwa ...jambo hilo sio kweli," amesema.
"Mbowe anafahamu katika mapendekezo 84 yaliyotolewa mapendekezo 63 yote yamechukuliwa na yapo kwenye mswaada ambao hatua za kisheria zinaendelea katika kuundwa kwa sheria na yeye ni mnufaika mkubwa wa maridhiano ambayo yamemfanya akawa yupo huru na kesi zote za kisiasa kuachiwa huru bila masharti na yeye mwenyewe na chama chake na vingine kufanya mikutano ya hadhara bila kubugudhiwa tena kwa ulinzi mkali chini ya Jeshi la Polisi kuhkikisha dhamira ya Rais Samia inatimia si tu kwa vyama vya siasa bali kwa Watanzania wote," amesema.









