Mavunde ameyasema hayo jana katika eneo la Nyerere Square wakati wa zoezi la kugawa majiko na mitungi ya gesi 500 kwa Mama Lishe na Baba Lishe wa Jijini Dodoma kutoka kampuni ya ORYX.
“Tunaishukuru Serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa nyingi za kiuchumi zitokanazo na shughuli mbalimbali kufuatia serikali kuhamia Dodoma, ni nafasi ya kipekee ambayo wanadodoma tunapaswa kuichangamkia badala ya kuwa watazamaji wa fursa."
"Niwashukuru kampuni ya ORYX kwa kusaidia upatikanaji wa majiko 500 kwa ajili ya Wanadodoma,hii ni hatua kubwa ya kusaidia kupunguza athari za mazingira zitokanazo na matumizi ya mkaa na kuni,"amesema.