Jengo hilo lilijengwa na kampuni ya Umoja na Sons ltd, P.o Box Mpanda- Katavi kwa gharama ya Sh. milioni 896.7 na ujenzi wake ulianza Machi mosi mwaka jana na kukamilika Novemba 30 mwaka huo na litakuwa na linauwezo wa kubeba abiria 200 kulinganisha na lile la awali lililokuwa likibeba abiria 25 pekee.
Amesema, jengo hilo linatarajia kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi katika eneo hilo, na linajumuisha sehemu ya kuwasilina kuondoka, sebule ya watu mashuhuri na chumba cha mikutano, duka la kahawa, zawadi pamoja na huduma kwa watu wenye ulemavu.
Dk. Bristow amesema, Mgodi wa Buzwagi ulikuwa wa pili kwa ukubwa nchini na uliajiri zaidi ya watu 3,000 na maisha ya uendeshaji yalifikia tamati julai 2021na ulifungwa rasmi julai 2022. Hivyo wanahakikisha wanaacha urithi mzuri ambao utakuwa endelevu kwa jamii kwa muda mrefu hasa kwenye sekta ya afya, elimu na kilimo.
Awali akipokea jengo hilo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme alisema, aliwapongeza Barrick kwa kutumia sehemu ya mapato yao kujenga jengo la kisasa la abiria ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na kuwataka TAA kulitunza ili kuwa na kumbukumbu ya Mgodi huo kwa kile ilichofanya baada ya kufunga uzalishaji.
Hata hivyo alimuomba Rais huyo kutuma timu na kwenda kufanya utafiti wa madini katika Wilaya ya Kishipu ili kuendelea na uchimbaji wa madini, kwani mkoa wa shinyanga unamaeneo makubwa yenye madini na yanahitaji utafiti.