Akisoma shtaka hilo mbela ya hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Tumsifu Barnabas mwendesha mashtaka wa Polisi Mkaguzi wa Polisi Martha Chacha amewataja washtakiwa wengine kuwa ni Majaliwa Damasi, (18) Mkazi wa Masumbwe, Emmanuel Damasi, (34) Mkazi wa Bulungwa , Selina Mchele (49) Mkazi wa Lwenge, pamoja na Maneno Mashauri (19) naye Mkazi wa Lwenge.
Martha ameiambia Mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Oktoba 12, 2023 huko Lwenge wilayani Sengerema kwa kumuua Sophia Maduka (61) na mmewe Mathias Lusesa (73) wote wakazi wa Lwenge wilayani humo kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Hata hivyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na kurejeshwa rumande kutokana na Mahakama hiyo kukosa Mamlaka kisheria ya kusiliza shauri hilo.
Hakimu Barnabas ameahilisha kesi hiyo hadi Februari Mosi, 2024 kwaajili ya kutajwa.