Mavunde ahamasisha wananchi Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi

14Jan 2024
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Mavunde ahamasisha wananchi Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali wa Jiji la Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo Dodoma na hasa kuzingatia ukuaji wa kasi wa Jiji baada ya maamuzi ya serikali kuhamishia shughuli zake zote Dodoma.

Mavunde ameyasema hayo jana katika eneo la Nyerere Square wakati wa zoezi la kugawa majiko na mitungi ya gesi 500 kwa Mama Lishe na Baba Lishe wa Jijini Dodoma kutoka kampuni ya ORYX. 

 

“Tunaishukuru Serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa nyingi za kiuchumi zitokanazo na shughuli mbalimbali kufuatia serikali kuhamia Dodoma, ni nafasi ya kipekee ambayo wanadodoma tunapaswa kuichangamkia badala ya kuwa watazamaji wa fursa."

 

"Niwashukuru kampuni ya ORYX kwa kusaidia upatikanaji wa majiko 500 kwa ajili ya Wanadodoma,hii ni hatua kubwa ya kusaidia kupunguza athari za mazingira zitokanazo na matumizi ya mkaa na kuni,"amesema.