"Hali ya Matumizi ya Dawa za Kulevya kwa wanafunzi wa Chuo ipo kwa kiwango cha wastani; zimeripotiwa kesi mbalimbali za wanafunzi walioingia katika uraibu wa dawa za kulevya" amesema Miraji.
Aidha ameeleza kuwa kuwepo kwa athari mbalimbali zinazoweza kutokea kutokana na Matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo tatizo la afya ya akili pamoja na vitendo vya Rushwa kwa watumiaji.
"Mafunzo hayo yaliambatana na shuhuda kutoka kwa aliyewahi kuwa mraibu wa dawa za kulevya kutokea Asasi ya Kimara Peer Educators akielezea athari alizokutana nazo kipindi akiwa anatumia dawa hizo,na kuwahasa wanafunzi hao kutojihusisha na Matumizi ya dawa hizo" jina limehifadhiwa.
" Mamlaka hiyo(DCEA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, Mratibu wa Afya ya Akili Halimashauri ya Wilaya ya Arusha pamoja na Asasi ya kiraia Kimara Peer Educators ilitoa elimu juu ya madhara ya matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa wananafunzi 230 wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kilichopo Sakina" amesema Miraji.