Shonza ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma baada ya kufanya kikao na msanii huyo na kumuhakikishia kuwa kwa sasa amebadilika na anataka kuionyesha jamii kuwa amefanikiwa kujikwamua katika matumizi ya madawa ya kulevya na hataki tena kwani anazaidi ya miezi mitatu sasa hajatumia madawa hayo.
“Kati ya wasanii wenye kukubalika na mashabiki wewe Chid benz ni mmoja wao na shabiki zako ni wengi hivyo ningependa kukuona kuanzia sasa unalijenga zaidi jina lako kwa kuonyesha kuwa umebadilika na nitafurahi zaidi kukuona unasonga mbele na hurudi tena katika matumizi ya madawa ya kulevya na Wizara ipo pamoja na wewe kukusaidia wakati wowote,”amesema Shonza.
Naye Msanii huyo wa Bongofleva Chid benz amesema kuwa kwa sasa hautarudi nyuma tena sababu tayari amekwisha acha kutumia madawa hayo na pia ataitumia bahati hii kuwafurahisha mashabiki wake ili waendelee kuukubali muziki wake.
Aidha, Chidibenz ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumpa ushirikiano wa haraka katika kazi zake kwani anaona huu ndo wakati wa kuwafurahisha mashabiki zake.
“Ombi langu kwa serikali ni kupata ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao Beautiful ambao nimeuiamba nikisifu uzuri wa mwanamke na kufuatia janga la Corona ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili ya Corona ,”Chid benz.










