Wasanii kutoka visiwani hapa, Siti & the Band waliweza kuonyesha uwezo wao wa kupiga muziki wa asili wa Afrika pamoja na muziki wa mwambao (taarab) na aina ya rege ambao uliamsha shangwe nara zote wa mashabiki wa muziki waliofurika Ngome Kongwe.
Pia kundi la Tara Jazz ambao nao wanatokea visiwani hapa waliweza kuamsha shangwe kwa nyimbo zao zilizokuwa na mchanganyiko wa afro jazz ya asilia ya kiafrika.
Msanii wa kutoka Kenya, Lulu Abdalla naye aliwasha moto mkali kattika jukwaa hilo alipopanda na bendi yake kwa mziki wa asili ya Afrika uliojaa vionjo mbalimbali vya asili.

Msanii huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali kupitia albam yake ya 'Thembassa' ya 2014, alipagawisha umati mkubwa.
Mwanadada kutoka Senegal, Thais Diarra aliweza kuonyesha umahiri wake wa kuimba muziki wa uliochanganywa na vionjo vya ala za asili ya Afrika Magharibi. Ndani ya Ngome Kongwe umati mkubwa ulifurika kushuhudia tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la 17 kutokea kuanzishwa kwakwe.











