Harmonize: Wanawake wengi wananipenda

29Dec 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Harmonize: Wanawake wengi wananipenda

NYOTA wa muziki wa Bongofleva na mkuu wa lebo ya Konde Worldwide, Harmonize, ameibuka na jipya kuhusu wanawake wengi kumzimikia ikiwa imepita wiki chache baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake na meneja, Kajala Masanja.

Harmonize.

Kupitia Instagram, Harmonize amesema katika siku za hivi karibuni tangu wasikie habari yuko singo baada ya msalaba wake aliosema hadharani  ataubeba kumwelemea, wanawake wengi wameanza kumvizia.

Msanii huyo hata yeye alikiri amechanganyikiwa ni kwa nini wanawake wanamfuata kila kona huku akikisia huenda ni kwa sababu ya nyota ya mafanikio yake kila uchao.

“Nimechanganyikiwa katika hili…wanawake siku hizi wananipenda kupita maelezo asikwambie mtu.

“Ni kwa sababu naendelea kupaa kiutajiri au pengine ni kutokana na utanashati wangu,” aliandika Harmonize.