Penzi la Wema, Whozu chali

29Dec 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Penzi la Wema, Whozu chali

PENZI la Wema Sepetu na msanii, Whozu linadaiwa kwa sasa halipo tena na kila mmoja ameshika hamsini zake.

Wawili hao wanadaiwa kuachana na Wema alianza kuposti snapchat anatamani kufa.

Katika mwendelezo huo huo amefuta picha zote za Whozu ambazo amewahi kuzipost kwenye page yake.

Hii ni dalili tosha wawili hao hawapo pamoja tena na mbaya zaidi Wema amepost video akicheza na mwanaume mwingine.

Mara kadhaa mrembo huyo wa Tanzania alishinda taji katika shindano la mwaka 2006, huweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi na anapoachana na mpenzi husika, pia huweka hadharani.