Kupitia Instagram, Harmonize amesema katika siku za hivi karibuni tangu wasikie habari yuko singo baada ya msalaba wake aliosema hadharani ataubeba kumwelemea, wanawake wengi wameanza kumvizia.
Msanii huyo hata yeye alikiri amechanganyikiwa ni kwa nini wanawake wanamfuata kila kona huku akikisia huenda ni kwa sababu ya nyota ya mafanikio yake kila uchao.
“Nimechanganyikiwa katika hili…wanawake siku hizi wananipenda kupita maelezo asikwambie mtu.
“Ni kwa sababu naendelea kupaa kiutajiri au pengine ni kutokana na utanashati wangu,” aliandika Harmonize.









