Diamond: Sina  roho mbaya

02Jan 2023
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Diamond: Sina  roho mbaya

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimtaja kama mmoja wa wasanii wasiopenda maendeleo ya wenziwe na hata kumtaja kuwa mwenye roho mbaya.

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Diamond ameweka bayana kuwa anafahamu wapo watu wenye kuamini kuwa ameshiriki kukwamisha jitihada na mipango ya baadhi ya wasanii kiasi cha wengine kumuona kama mtu asiyependa maendeleo ya wengine.

Jambo alilolikanusha kwa kuweka wazi uhalisia wa maisha yake na namna anavyopenda kushiriki katika kuhakikisha anaunga mkono jitihada za wasanii wengine.

“Mimi siamini kwamba mtu mwingine akifanikiwa ndio mimi nitafeli, hapana, watu wakati mwingine naona wanaandika kwenye mtandao kwamba ninaroho mbaya, lakini sijawahi kuwa na roho mbaya,” alisema.

“Kwa sababu mimi naweza kusema ndio msanii ambaye nimetoa wasanii wengi wenye nguvu katika nchi hii, na sijawahi kuwa na tatizo na mtu, labda tu unaweza kusikia wachonganishi wakizungumza mambo ambayo baadaye yanakuja kuwa chuki.

“Na siku hizi ninasapoti kazi zao, napenda kushiriki, napenda kuona ifanikiwe kwa sababu naamini kwa namna moja au nyingine muziki ni maisha ya watu, akifanikiwa mtu unakuwa umemkomboa kimaisha,” alisema Diamond.