Kiki Zimba awa gumzo Swahili Fashion 2022

09Dec 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kiki Zimba awa gumzo Swahili Fashion 2022

MBUNIFU wa mavazi mahiri nchini, Kiki Zimba amekuwa gumzo kwenye onesho la Mitindo la  Swahili Fashion 2022 kutokana na ubunifu wa vazi lake lililoonesha Mlima Kilimanjaro ambalo lilivutia wageni wengi.

Akizungumzia kuhusiana na vazi hilo, Kiki alisema: "Dhumuni la kubuni vazi hili ni kuutangaza Mlima Kilimanjaro kwa kuwa mwezi Septemba mwaka huu  nilipanda na kujikuta nikivutiwa na mazingira ya mlima huo yaani hata watalii wanaupenda sana ndo maana ujumbe wangu kupitia 'fashion' hasa kwenye Swahili Fashion 2022 ni kuwataka Watanzania na wageni kuupanda mlima huo,” alisema Kiki.

Zimba aliingia kufanya onesho siku ya mwisho siku ambayo wabunifu mahiri hufunga maonesho hayo.

Wanamitindo walionesha mavazi mbalimbali yakiwemo ya kutokea kwenye dhifa za kila aina.