Watoto wa wafugaji wakata ‘minyoyoro’ na kuchangamkia elimu

26Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Watoto wa wafugaji wakata ‘minyoyoro’ na kuchangamkia elimu

Jonathan Tipapa ana umri wa miaka tisa.Kila siku anafanya safari ya kwenda na kutoka shule.Anakabiliana na hatari nyingi ambazo zilikaribia kumfanya akaribie kuacha shule – kama ilivyotokea kwa rafiki zake wengi ambao sasa wanaweza kuonekana wanachunga ng’ombe hata katika siku za shule.

Jonathan Tipapa ana umri wa miaka tisa.Kila siku anafanya safari ya kwenda na kutoka shule.

Anakabiliana na hatari nyingi ambazo zilikaribia kumfanya akaribie kuacha shule – kama ilivyotokea kwa rafiki zake wengi ambao sasa wanaweza kuonekana wanachunga ng’ombe hata katika siku za shule.

Yeye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Enkutoto katika Jimbo Narok Kusini katika mkoa wa Rift Valley, takriban maili 70 kutoka mji mkuu wa Nairobi.

"Mimi huondoka nyumbani kukiwa bado giza na kutembea kwenda shule peke yangu, jirani yetu wa karibu anaishi mbali sana kutoka nyumba yetu hivyo mimi sina mtu wa kutembea naye. Mimi naogopa giza, wakati mwingine huwa naogopa kukanyaga nyoka ninapotembea msituni u, " Tipapa aliiambia IPS, akiongeza kuwa yeye kamwe hawezi kuondoka nyumbani bila ya kushika fimbo mkononi.

Kijiji chake mara nyingi hukumbwa na mgogoro kati ya binadamu na wanyama pori.. Lakini fimbo yake ndogo haiwezi kuwakabili wanyama kama tembo ambao wamekuwa wakifahamika kwa tabia zao za wanazurura kupitia katika kijiji chake au mafuriko ambayo huvamia mkoa wao bila ya taarifa.

Simulizi hii inayowahusu watoto wengi wa Kimasai katika harakati za kutafuta elimu.Wanatembea umbali mrefu kutoka nyumbani kwao hadi shuleni.Umbali huo ni mrefu sana kwa kijana mwenye umri kama huo.

Marafiki wa Tipapa hawaendi shule kama yeye. Hutumia siku zao katika mashamba ya malisho ya mifugo. Wasichana husaidia kazi za nyumbani wengine huwatunza watoto wao wadogo waliojifungua wakiwa watoto Hii haitokani na ukosefu wa karo ya shule kwa sababu elimu ya msingi inatolewa bure na ya lazima katika taifa hilo la Afrika Mashariki tangu mwaka 2003.

Mamilioni ya watoto kutoka katika familia maskini wamenufaika na mpango wa elimu bure. Hata hivyo, hii ni, tofauti kabisa kwa watoto wanaokulia katika jamii zilizotengwa za wafugaji..

Lakini simulizi hii inabadilika taratibu. Bernard O Sankale, mwalimu mkuu wa Elangata Enterit shule ya msingi ya bweni katika Narok Kusini’ aliiambia IPS kuwa, kuenea kwa shule za bweni za msingi huko Narok Kusini kuongeza msukumo katika sekta ya elimu kutokana na ukweli kuwa zinahitajika sana katika jamii ya wafugaji.

"Huduma za bweni ni ufumbuzi wa matatizo zaidi ambayo tunakabiliana nayo.

Umbali daima umekuwa ni kikwazo kikubwa. Wengi huchoka sana kutembea umbali wa kilomita nyingi kwenda na kutoka shule na kujikuta wakilazimika kuacha, "anasema. Kuna wanafunzi 477 katika shule hii ambao angalau 160 kati yao wananufaika na huduma za bweni.

Shule nyingi hutoa huduma ya bweni kwa wanafunzi ambao angalau wana umri wa miaka 10 kwa sababu wanaweza kujihudumia wenyewe na wanaweza kukabiliana na mazingira ya kuwa mbali na familia zao. Wazazi wanachotakiwa ni kulipa ruzuku ya ada dola za Marekani $ 45 kwa mwaka ili kuwafanya watoto wao wafurahie huduma za bweni katika shule hizo.

Matokeo yake, ni kwamba shule hiyo itakuwa na idadi kubwa kabisa ya watahiniwa ambao wanatarajia kufanya mtihani kwa ajili ya Cheti cha Elimu ya msingi cha Kenya (KCPE) baadaye mwaka huu.

"Tuna watahiniwa 60 na 22 kati yao ni wasichana, hii ni mara mbili idadi ya wasichana waliofanya mtihani wa taifa mwaka jana," alifafanua.

Rekodi za shule zinaonyesha kuwa idadi ya wasichana waliofanya mtihani wa KCPE - mtihani wa taifa ambao ni wa lazima kwa wanafunzi wote kuufanya ili kuwawezesha kujiunga na shule za sekondari - imekuwa ikipanda juu ya kupanda.

shule imetoka katika hali ya kutokuwa na mwanafunzi wa kike hata mmoja aliyefanya mtihani mwaka 2007 hadi wasichana 22 mwaka huu.

"Lakini si tu kuwa na huduma za bweni kituo,jumuiya inachotakiwa ni kuunga mkono kituo hiki kwamba ambacho kinafanya tofauti kwa wote," Sankale alielezea. "Wazazi wanapokuwa tayari kuwaweka watoto wao katika shule, wanafunzi wetu walianza kulala katika madarasa na ofisi ya Mwalimu Mkuu kwa ukosefu wa mabweni mwaka 2009. Tulikuwa tunaweza kuwahifadhi wachache sana wakati huo," aliongeza.

Kwa mujibu wa Christine Orono, mwenyekiti wa bodi wa World Vision Kenya kwamba inasaidia wanaoishi katika mazingira magumu kuweza kupata elimu bora, shule za msingi za bweni za umma ni kutumikia kama vituo vya uokoaji kwa wasichana. "Wasichana ni salama kutoka tamaduni mbaya kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni na mimba za utotoni," anasema.

Sankale anasema kwamba, ni rahisi sana kuoa msichana ambaye hahudhurii shule. Wavulana pia watajiepusha na utamaduni wa madhara ya ushujaa wa kivita ambao wao hutengwa na kuwekwa katika vichaka kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya kuwa mashujaa.

Katika kipindi hiki, wao hujiingiza katika vitendo vya vurugu mbalimbali kama vile wizi wa ng'ombe na hivyo kujikuta wengi wamejeruhiwa na kufa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.

"Shule za Bweni pia zinafanya vizuri ukilinganisha na shule za kutwa. Wanafunzi hutembea umbali mrefu pia kusaidia kazi za nyumbani jioni hawezi kufanya kwa kiwango chao bora, "anaelezea Peter Saitoti, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Enkutoto. Umbali wa kilomita tisa ipo Elangata Enterit shule ya bweni ya msingi.

Mwaka 2014, shule ilifanywa kuwa ya kwanza katika divisheni hiyo kati ya shule 23 na namba moja katika wilaya yake katika shule 189.

Saitoti hata hivyo anasema kwamba shule yake bweni inapokea wavulana tu wakati huu. "Ingawa shule zetu zote katika mkoa huu zina wavulana kuliko wasichana,alibainisha kuwa idadi ya wavulana inapunguza kama ile ya wasichana inaendelea kuongezeka hivyo kuna haja ya kwanza kujibu mahitaji ya mtoto mvulana," alfafanua.

Kulingana na yeye, kuna wanafunzi 474 katika shule, 259 ni wavulana na 215 ni wasichana katika darasa la nane, idadi ya wavulana ni sawa na ile ya wasichana:

"Haya ni maendeleo mazuri lakini wasiwasi wetu ni kwamba, idadi ya wavulana kuacha shule inaongezeka wakati wasichana wanaongezeka zaidi kukaa shule." Wakati ambao shule zaidi na zaidi za msingi zinawekeza katika mabweni, kuna matumaini mapya kwamba mtoto wa Kimasai atashinda vikwazo hivyo kuingia darasani.