Wageni warejesha kipindupindu Iringa baada ya ukimya miaka 10

10Mar 2016
George Tarimo
Dar
Nipashe
Wageni warejesha kipindupindu Iringa baada ya ukimya miaka 10

Ni mapigo mawili ya athari za afya na mazingira yanayowkabilia wakazi wa Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

Mafuriko yatokanayo na mvua zinazonyesha katika kipindi kilichopo na janga la kuvamiwa na ugonjwa wa kipindupindu.

Hadi mwishoni mwa mwaka uliopita, kuibuka kipindupindu kumeibua mshangao kutoka kwa wakazi na uongozi wa mkoa, kwamba maradhi hayo yameibuka baada ya miaka 10 kupita ikiwa imedhibitiwa.

Hadi wiki moja na nusu iliyopita, ripoti inaonyesha kuwa janga lililojitokeza limeshaua mtu mmoja na wengine 85 wanaugua.

Ripoti hiyo kutoka Zahanati ya St Lucas Mboliboli, ambako kuna kambi ya matibabu, ugonjwa uripotiwa hapo kwa mara kwanza, Februari 6 mwaka huu.

Inaelezwa kuwa, sehemu zilizoathrikla ni kijiji cha Mbolimboli kilichopo katika katika Tarafa ya Pawaga, Jimbo la Isimani.

KAULI YA RC

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, anafafanua kuwa kipindupindu hicho kimesababishwa na vibarua ambao ni wageni katika mkoa huo walioajiriwa kwenye mashamba ya mpunga eneo la Pawaga, ndio chanzo kikuu.

Anasema, wafanyakazi hao wa mashambani walioko Pawaga, eneo ambalo limeathirika na mafuriko, wanatoka katika maeneo tofauti.

Mkuu wa Mkoa anasema waathirika hao wa kipindupindu wanatoka katika Halamshauri ya Wilaya ya Kilolo, hasa katika eneo la Ilula, mkoani Dodoma, pamoja na wenyeji wachache wa Pawaga.
Jingine analosema ni kwamba, mashamba hayo yanayolimwa kwa kutumia vibarua, yameathirika na kipundupindu kutokana na majaruba ya mpunga kutumiwa na vibarua kama vyoo, katika makazi yao ya muda shambani.

Mkuu huyo wa mkoa anataja hicho ndicho chanzo cha mlipuko wa kipindupindu kupitia maji yanayosambaa shambani.

Amina anawatahadharisha wananchi na hasa wakazi wa mashambani, kuwa makini dhidi ya uchafu kwa kuweka umuhimu wa jamii kuwa na vyoo, jambo litakalowaengua kutoka tabia ya kujisaidia shambani.

Kwa mujibu wa Amina, udhaifu huo ndio ulioko kwa vibarua waliowagundua wana mazoea ya kula bila ya kunawa mikono, huku baadhi ya vyakula hivyo havijachemshwa

Jingine analolifafanua mkuu huyo wa mkoa katika tafsiri ya utaalam wa afya, ni kwamba vimelea hivyo vinaweza kukaa kwenye mwili wa binadamu ndani ya siku saba.

Mkuu wa Mkoa anasema katika mazingira hayo, ni rahisi athari kulipuka mwilini mwa mtu ambaye kinga yake ni ndogo

Mbali na uchafuzi wa majaluba ya mpunga, pia mafuriko yanabomoa vyoo na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya kusambaa kipindupindu.

“Tumeanzisha kambi ya kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu katika Zahanati ya St.Lucas katika kijiji cha Mboliboli na wataalam wa afya wamepelekwa vifaa tiba,” anafafanua Amina.

Anaongeza: “Vipo vya kutosha kwa ajili ya tiba na kwamba bado serikali inaendelea kuhakikisha wagonjwa wote wanahudumia katika zahanati hiyo.”

Mkuu wa mkoa anafafanua kasi ya maambukizi inachangiwa na watu ama kula au kunywa matapishi yao kwa njia mbalimbali, ikiwemo kunywa maji machafu.

Anasema vifo vingi vinatokea kutokana na ucheleweshaji wa wagonjwa kwa ajili ya tiba.

Pia mkuu wa mkoa analalamika kuhusiana na watu kukosa vyoo ba na bafu na yale yaliyopo ni machafu na kugeuka vyanzo vya kusambaa kipindupindu.

UDHIBITI WA MKOA

Anasema mikakati ya kudhibiti kipindupindu Iringa imefanyika kwa kufungua kambi maalum ya matibabu katika zahanati ya St Lucas iliyoko katika kijiji cha Mboliboli.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe, anawaagiza wafanyabiashara wa chakula na matunda kusimisha kwa kwa muda shughuli hizo, ili kupisha vita dhidi ya kipindupindu.

“Kama mlikuwa hamjui, Manispaa ya Iringa ni lango. Watu waliopo Pawaga wanakuja mjini kununua bidhaa mbalimbali, hivyo ni vyema tukajihami kabla ugonjwa huo haujafika. Tukichelewa,athari yake inaweza kuwa kubwa kuliko ilivyo katika maeneo mengine,” anatahadharishaa Meya Kimbe.

Pia amepiga marufuku unywaji pombe kwenye maeneo yaliyoathirika.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Stephen Muhapa, anasema hahitaji mzaha katika vita ya kuikabili kipindupindu iliyopo kwenye halmashauri yake na inawahusu wananchi wote.

“Ugonjwa huu unaua kwa haraka kuliko ugonjwa mwingine. Tusiingize ugonjwa huu na mambo ya kisiasa, katika hili siasa weka mbali

“Jambo hili ni letu sote kuhakikisha tunapambanana nao hadi mwisho kuhakikisha watu wote wanapona,”antamka Muhapa.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk. Robert Salim,. Anawataka wananchi mkoa kwake kutoa taarifa ya haraka mtu anapojigundua au kugunduliwa na kipindupindu, ili madaktari walioandaliwa wamfuate aliko.