Tambua majaabu ya kidonge cha Aspirin katika afya yako

10Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
Tambua majaabu ya kidonge cha Aspirin katika afya yako

ASPIRIN ambayo wataalam sasa wanaiita ‘Dawa ya Milenia’ imebainika kufanya maajabu mengi kutokana na uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali.

Kidonge cha Asprin.

Kwanza, Asprin hupatikana kwa bei nafuu huku ikiwa na athari ndogo kwa mtumiaji. Hivi sasa inatumiwa na mamilioni ya watu duniani kote kwa mengi.

Miongoni mwa matumizi na manufaa ya dawa hiyo, ni kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack), kupooza (stroke), kurutubisha mfumo wa uzazi na uchovu (hangover).

Taarifa ya kitaalam ya hivi karibuni, imebaini kuwa Aspirin inazuia ugonjwa wa saratani, huku ikiwa na mchango mwingine wa kusaidia urutubishaji mfumo wa uzazi na kutibu tatizo la akili.

Wiki iliyopita, kliniki kubwa ya majaribio ya magonjwa duniani ilizindua uchunguzi wa dawa ya Aspirin, kuchunguza namna inavyoweza kutibu au kuzuia saratani za tumbo, matiti, koo na kibofu cha mkojo.

Uchunguzi huo umepangwa kuhusisha watu 1,000 ambao watatumia Aspirin na kazi hiyo imefadhiliwa na Taasisi ya Utafiti wa Saratani ya Uingereza na zinginezo. Ni utafiti unaotarajiwa kuchukua miaka 12, kabla ya kupata majumuisho ya mwisho.

UTAFITI MAREKANI
Wakati huo huo, utafiti unaofanyika nchini Marekani, umegundua kwamba kutumia takriban robo ya Aspirin kila siku, kunaweza kumpa mwanamke nafasi kubwa ya kupata ujauzito na mtoto mwenye afya njema.

Kuna majaribio mengine ya kliniki kubwa duniani yanaendelea na yanatarajiwa kutoa matokeo ya nafasi ya Aspirin kwa muongo mmoja ujao.

Taarifa njema ni kwamba, mwezi Agosti mwaka jana, utafiti ulibaini kwamba kutumia dozi ya Aspirin kila siku, kunaokoa maisha ya watu zaidi ya 6,500.

Inaelezwa kuwa, hiyo inatokana na ukweli kwamba takriban kila mwaka saratani huathiri wastani wa watu 500 kwa mwaka.

TAHADHARI
Hata hivyo, kuna tahadhari kuhusu matumizi ya Aspirin. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Queen Mary cha London, Uingereza, umeripoti madhara ya dawa hiyo kwamba ni pamoja na kutokwa damu na vidonda vya tumbo.

Ripoti ya utafiti huo inasema kuwa, madhara hayo yamesabisha vifo vya takriban watu 900 kwa mwaka nchini Uingereza na wataalam hao wanaonya kuwa mtu anayetaka kutumia Aspirin, anapaswa kupata ushauri wa daktari kwanza.

KUZUIA SARATANI
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha London, Profesa Ruth Langley, anabainisha kuwa katika majaribio ya kuangalia matumizi ya dozi ndogo ya Aspirin, imebainika inawasaidia wagonjwa wa moyo.

“Watafiti wamebaini kusambaa taratibu kwa ugonjwa wa saratani, pia watu wachache walifariki kutokana na saratani,” anasema Profesa Langley, ambaye ni Mtafiti Mkuu wa Majaribio ya Aspirin chuoni hapo.

Katika utafiti wa kihistoria uliichapishwa katika jarida la The Lancet mwaka 2011, kazi iliyoongozwa na Profesa Peter Rothwell wa Chuo Kikuu cha Oxford una mengi kwa afya ya mtumiaji Aspirini.

Ripoti hiyo inasema kuwa, dawa hiyo angalau miaka mitano katika umri wa kati, kunapunguza hatari ya kupata saratani ya tumbo, koo na kibofu kwa asilimia 20, pia inalinda mtumiaji dhidi ya saratani za matiti, mapafu na kibofu.

“Wagonjwa wa saratani wanaotumia Aspirin kila siku, wana uwezekano wa kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo kwa asilimia 30 hadi 40,” utafiti zaidi wa timu ya Profesa Rothwell unafafanua kupitia ripoti yake.

INAFANYAJE KAZI?
Jibu ni kwamba aspirin inapoingia kwenye damu inachembe kadhaa zinazonata kwenye damu hivyo kuzuia uwezekano wa damu yako kuganda.

Kwa mujibu wa Prof. Langley, chembe zinazotajwa kuwa kwenye Aspirin zinazojulikana kama ‘Platelets’ zina uwezo wa kunasa kwenye seli za saratani na zinapunguza uwezo wa kinga ya mwili kufanya kazi.

NANI WA KUMEZA ASPIRIN?
Profesa Rothwell anashauri kwamba, iwapo mtu anatoka kwenye familia yenye historia ya saratani ya tumbo au koo na umewahi kupima na kubainika kuwa na vimelea vya ugonjwa huo hivyo, dawa hiyo inamhusu.

URUTUBISHAJI
Wiki iliyopita, wataalam wa afya ya uzazi walipendekeza kuwa kwa wanawake ‘wanaotafuta’ watoto wajaribu kutumia Aspirin kila siku, wakiiita dawa hiyo kuwa ‘dawa ya Milenia.’

Profesa Richard Paulson wa Taasisi ya Afya ya Uzazi ya Marekani, katika majibu kwa utafiti mpya kutoka Chuo Kikuu cha Utah uliobaini kuwa mwanawake anayemeza karibu robo ya aspirin (81 mg), alikuwa na uwezekano mkubwa wa kushika mimba na kujifungua salama.

Utafiti huo ulliwahusisha wanawake 1,228 waliopata tatizo la kuharibika kwa mimba katika miezi 12 kabla ya utafiti.

NANI AMEZE NA
INAFANYAJE KAZI?
Watafiti wanasema kuwa, kunywa kidonge cha Aspirin kila siku, kunafanya kazi ya kupunguza kuvimba kizazi na kufanya maandalizi kwenye tumbo la uzazi kupokea na kutunza mtoto.

Mwanamke wenye uwezo mkubwa wa kuvimba kizazi na anatafuta kupata ujauzito, wanaweza kunufaika, anasema Dk. Nick Raine-Fenning, mshauri wa magonjwa ya wanawake kutoka Nottingham, Uingereza na msemaji wa Chuo cha Wakunga na Madaktari wa Wanawake cha Royal.

Anashauri kwamba wanawake wenye tatizo hilo, wanapaswa kupata ushauri kwanza wa kitaalam kutoka kwa madaktari wao, kabla ya kuanza kutumia Aspirin.

Pia anashauri kuwa, matumizi ya Aspirin kila siku, kunaweza kuwaondoa wajawazito katika hatari ya kujifungua kabla ya wakati.

Inaelezwa kuwa, asilimia nane ya mimba zinazohairibika au kujifungua kabla ya wakati, inasababishwa na shinikizo la damu wakati wa ujauzito.

Dk. Nick anasema Aspirin inaweza kutumiwa na wanawake wenye tatizo la kuganda damu, ambalo ni la hatari ya kuharibika kwa ujauzito

SHAMBULIO LA MOYO
Kwa mujibu wa Kituo cha taarifa za afya ya jamii, takriban matumizi ya Aspirin milioni 30 yaliripotiwa mwaka 2014 kwa wagonjwa wa moyo, ili kuwasaidia kuzuia kujirudia kwa mshtuko wa moyo au kiharusi.

“Kwa wale walio na ugonjwa wa moyo, kuna uthibitisho wa uhakika kwamba kumeza aspirin kila siku, kunaweza kupunguza hatari ya kupata shambulio zaidi la moyo,” anasema Dk. Vinay Bhatia, Mshauri wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Spire Tunbridge Wells ya Uingereza.

“Aspirin inalainisha damu na husaidia kuizuia kuganda katika mishipa ya damu. Kuganda kwa damu kunasababisha mashambulizi ya moyo, kwa kusitisha usambazaji wa Oksijeni kwa misuli ya moyo," anasema Dk. Bhatia.

Aidha, Mkurugenzi Mwandamizi wa Mfuko wa Moyo ya Uingereza Dk. Mike Knapton, anasema: "Kama una magonjwa ya moyo au uliwahi kupata shinikizo la moyo, kumeza kiwango cha chini cha Aspirin (Milgram 75) kila siku hupunguza hatari ya kujirudia kwa ugonjwa huo kwa mara nyingine.

“Kama uliwahi kupata shinikizo la moyo, kutafuna Milligram 300 za Aspirin unaweza kupunguza hatari ya kufa kwa asilimia 25,” anafafanua Dk. Knapton na kuweka angalizo: “Lakini usianze tu kumeza Aspirin, wasiliana kwanza na daktari wako.”

KIHARUSI
Katika kundi la watu 10 waliowahi kupatwa na shinikizo la damu, watatu kati yao wana uwezekano wa kupata shinikizo la dau.
Chama cha Wanaopatwa na Shinikizo la Damu, linasema imethibitika Aspirin kuwa na uwezo wa kudhibiti shinikizo la damu.
INAVYOFANYA KAZI
“Shinikizo la damu hutokea mara kwa mara, damu inpoganda katika mshipa mpana eneo la shingoni, ambayo inasababisha kupasuka kwa mishipa midogo kichwani,” anasema mtaalam Dk. Bhatia.

Anaongeza kuwa athari hiyo ya damu inaweza kutokea katika sehemu nyingine ya mwili na athari za moja kwa moja kujitokeza kichwani.

Kuna utafiti uliofanyika nchini Sweden, uligundua mtu mzima mwenye umri zaidi ya miaka 70, anayetumia Aspirini anakuwa salama kiafya.
Kwa kurejea uzoefu wa mtu huyo mzima aliyetumia dawa hizo kwa zaidi ya miaka mitano, kwamba, ilimfaa zaidi kiafya, ikilinganishwa na wengine wa umri huo wasiotumia Aspirin.

Kuna utafiti mwingine wa namna mbalimbnali unaofafanua kwamba, matumizi ya Aspirini yanachangia kudhibiti damu kuganda katika mfumo wa mishipa, ubongo na kichwani kwa jumla.

HATARI
Pamoja na sifa zote zilizoainishwa kuhusiana na matumzi ya Aspirin, kuna kundi la watu wachache wanaoathirika kwa kuwa kuwakwangua tumboni.

“Tuchukulie iwapo mtu atatumia Aspirin kwa miaka mitano, kati yao watu kati ya watano na 10 wanavuja damu puani,” anasema Profesa Rothwell.

Wakati katika sura hiyo ya athari ikigota katika hatau kwamba, asilimia 10 ya watumiaji Aspirini wanaweza kuteseka na maumivu makali tumboni.

Anaeleza kuwa, wanaopata athari za ubongo ni wastani wa mtu mmoja kati ya 10,000 ambao ni sawa na asilimia 0.0001.
Pia, kiwango cha athari kinaelezwa kupanda kuliganisha na umri wa mtu i unavyoongezeka na hasa unapodi miaka 70.

“Kwa baadhi ya mimba Aspirin inaweza kusababisha mimba kuharibika na damu kutoka,” anasema Dk. Raine-Fenning, anayeshauri kuwa matumizi ya Aspirini kwa muda mrefu, yanapaswa kuendana na ushauri wa daktari na katu isitumiwe kienyeji.

ASPRIN INATENGENEZWA NA NINI?
Ni dawa inayotokana na matumizi ya magome ya mti aina ya Willow. Iligunduliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na iantajwa na Wafamasia kuwa kidonge bira zaidi katika Karne ya 21.