Hiyo ni kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akitaja mafanikio ya serikali katika awamu iliyopo sasa, chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akisema utekelezaji wa miradi ya maji serikalini, kwa sasa ina dhamira ya kuhakikisha huduma ya maji mijini na vijijini inafika zaidi ya wastani wa asilimia 95 na 85, ifikapo mwaka 2025.Hapo anawashukuru washirika wa maendeleo,wakiwamo nchi rafiki, taasisi na mashirika ya kimataifa, kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kutoa huduma kwa wananchi.Ikumbukwe maji safi na salama, afya bora, pamoja na mazingira sahihi ni sehemu ya ubora ni mahitaji ya msingi ya binadamu, pia yana umuhimu kwa viumbe wote wanaoishi duniani, hata visivyo na uhai.Uhaba wa maji safi na salama, kimsingi ni chanzo cha uchafu wa mazingira, maradhi na chanzo cha migogoro, kama busara haitakuwapo kuvitunza. Inatajwa kuwapo ushahidi wa kitafiti, pale serikali na jamii, hazitasimama kidete kulinda, kutunza na kuendelezwa vyanzo vyake. Kimsingi, ni sehemu ya haki msingi za binadamu.Hadi sasa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wote bado ni changamoto, huku nchi zinazoendelea zikiathiriwa zaidi, Tanzania ikiwa sehemu yake. Hata ikirejewa, taarifa mojawapo ya Benki ya Dunia, inataja theluthi mbili ya Watanzania ndizo zinazopata huduma ya msingi ya maji.Ripoti zinathibitisha kutotosheleza huduma za maji na usafi (WASH), ikiwa ni kikwazo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hali ambayo pia inaangukia mwitikio wa Umoja wa Mataifa (UN), unapokubali maji na usafi wa mazingira, kama eneo linalohitaji uangalizi, wakati wa kuandaa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) mwaka 2015.Hadi sasa dhana ‘Maji na Usafi wa Mazingira’ yako chini ya lengo la sita la SDG, linalotaka kuhakikishwa upatikanaji uendelevu. usimamizi wa maji na usafi wa mazingira kwa wote.Mara nyingi, kutofikiwa na maji safi na salama, hata kuwa na athiri hasa kwa kinamama, ambao ndio wanaolazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya familia zao, ambayo katika sura ya pili, inabaki kuwa kikwazi kwao kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
SBL YAINGILIA KATI
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), katika utaratibu wa uwajibikaji wa kampuni, imeamua kuwekeza katika mipango ya huduma za maji na usafi, hasa kwa wanawake wilayani Handeni, mkoani Tanga.Mkurugenzi wa Uhusiano wa kampuni ya SBL, John Wanyancha, anataja nguzo mojawapo inayotumiwa na SBL, ni ushirikishaji, ikiwalenga wanawake kuwa kundi linaloonekana limesahaulika katika mradi huo, ni hatua ya kimkakati kuhakikisha kuna ushirikishwaji katika huduma za maji na usafi.Wanyancha anasema, SBL imewekeza kiasi cha Sh.milioni 25 ikiwagusa zaidi ya watu 2,000 wanaotarajiwa kunufaika, wakiwamo wanawake na watoto.Pia, anasema fedha hizo zitatumika kuwapa wanawake elimu inayohusiana na huduma za maji na usafi, pia ni akitaja ni mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Water Aid, ukitarajiwa kuanza wiki ijayo eneo la Kwamaizi Kampene, kata ya Kideleko wilayani Handeni.Mkurugenzi Wanyancha anafafanua: “Tuna shauku kubwa na mradi huu kwa sababu unagusa nguzo zetu mbili ambazo ni ‘Maji ya Uhai’…”
Kwa mujibu wa Wanyancha, ni mradi mwendelezo wa maji wa Sh.milioni 380 unaotekelezwa wilayani Handeni. Anafafanua: “Mwezi uliopita tulianzisha mradi mkubwa wa maji huko Handeni, kwa kuanza ukarabati na ujenzi wa bwawa la maji kwa kushirikiana na Wizara ya Maji, pamoja na msaada na serikali ya mtaa wa Handeni.“Baada ya hapo, tuliamua kimkakati kuanzisha mradi wa huu wa maji na usafi unaozingatia jinsia, ili kuwawezesha kundi lililotengwa huko Handeni na kwenye hili, sio wanawake tu kuendesha ajenda yetu ya ushirikishwaji, pia kuchangia kufikia lengo la sita la SDGs."
Anaongeza kuwa mradi wa Sh.milioni 25, una mana kwa wanawake eneo la Kwamaizi Handeni, kwamba watapata elimu inayohusiana na maji na usafi, hata kupata ufahamu wa kipengele cha fursa za ujasiriamali kwenye eneo hilo na uwekezaji.Manufaa mengine yanatajwa ni kupatikana mafunzo juu ya ustadi na utunzaji bustani unaojali mazingira, piaa ujuzi wa usimamizi wa fedha. "Ili kufanya mpango huo kuwa endelevu zaidi, wanawake watapewa pesa za kununua mbegu za mazao mbalimbali ili kuwawezesha kununua zana ambazo kwa madhumuni ya kuwekeza katika huduma za maji na usafi”.