Kamanda Mohamed wa TFS Kanda ya Ziwa asimulia ndani, nje vita vyao

27Apr 2023
Anthony Gervas
MWANZA
Nipashe
Kamanda Mohamed wa TFS Kanda ya Ziwa asimulia ndani, nje vita vyao
  • kuokoa misitu • Asali hawako nayo mbali… majangili nao ‘wanaipata’

TFS ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ambayo katika Kanda ya Ziwa iko katika juhudi na mipango mikakati yake, kupigania rasilimali za misitu na nyuki, pia kutunza mazingira.

 

Bakari Mohamed, ni Kamanda wa TFS Kanda ya Ziwa, pia akiwajibika kuwa Mhifadhi Mkuu wa Misitu, anaifafanulia Nipashe kuwa hadi sasa wana mpango unaoipa majukumu makubwa, ambayo kila baada ya miaka mitano wanafanyiwa tathmini, kulingana na mabadiliko ya kimazingira, teknolojia, uchumi, hali ya hewa na ikolojia.

Anataja miongoni mwa majukumu makubwa ambayo yako katika mpango mkakati huo, ni kuhifadhi na kuzilinda rasilimali za misitu na nyuki, zilizo katika hifadhi misitu ya taifa. Hapo anafafanua: “Kwa Kanda ya Ziwa, tunazo hifadhi za misitu zipatazo 24, sawa na hekta 415,000, ambazo tunahakikisha zinahifadhiwa, zinaendelea kulindwa, kuendelezwa, ili kuleta manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho kunufaika kiuchumi, kiikolojia na kimazingira.”

Katika mustakabali wa utamaduni, anadokeza kuwa ndani ya hifadhi kuna shughuli zilizorithiwa zikiendelezwa hadi sasa, katika kukuza mila na desturi za jamii ya Kitanzania, zikileta faida za kiuchumi kwa njia za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja kutoka katika misitu hiyo.

Mohamed anarejea katika uchumi, kwamba kuna manufaa ya kuwasaidia wananchi kupata mazao ya mbao kwa ajili ya shughuli za kijamiii, vilevile chakula, asali na dawa.

Pia, anataja suala la ikolojia ina manufaa kwa maisha ya binadamu na viumbe vingine, ikiismamia mazingira ya maisha. Hapo anafafanua kwamba mifumo ya kkolojia inagusa wanyama, mimea na wanyama, maji na hali ya hewa, huku kwa mwanadamu kuna mengi, maisha kwenda vizuri.

“Historia ya mistu na mwanadamu haiwezi kutenganishwa. Binadamu kwa miaka mingi, aliishi katika mistu, faida zake zilikuwapo tangu enzi na enzi, hivyo zitaendelezwa hadi leo,” anaeleza Mohamed.

Anabainisha kuwapo faida zingine ambazo ni kuvuta hali ya hewa, kusimamia joto duniani, kupunguza hewa ya ukaa angani, kuvuta mvua ambayo ina manufaa makubwa kwa viumbe hai, mfano kilimo kinavyotegemea mvua.

Pia, Mohamed anataja uvuvi na mifugo nazo zina faida za kijamii na kiuchumi, kiikolojia wananchi wanazitambua, kuzithamini, akieleza TFS Kanda ya Ziwa inalenga kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi ya mazingira na misitu yake, hata imeunda kitengo maalum cha kuelimisha umma umuhimu wa misitu.

Anasema katika mikoa mitano inayosimamiwa na TFS Kanda za Ziwa; Mwanza, Simiyu, Mara, Kagera na Geita, katika wilaya zake kuna maofisa hifadhi wa misitu, wanaoelimisha umma, pia  kulinda rasilimali za taifa, wakiwakumbusha wananchi kutambua faida hizo zisitoweke.

BUSTANI ZA MICHE

Jukumu lingine, Mohamed analitaja ni kuhakikisha wananchi wanapewa miche bora ya miti ya kupanda, ili kutunza mazingira yao iwe faida ya baadaye, kwa umma.

Kamanda Mohamed, anaeleza kuwa zipo bustani za miche ya miti ya kupanda inayozalishwa kutoka kwenye bustani zao,zilizopo katika mikoa yao ya kanda ya ziwa,ili kuweza kutunza mazingira.

TFS katika kanda hiyo kwa sasa, ina jumla ya bustani 10 za kuzalisha miche ya miti mbalimbali ikiwamo ya matunda, miche ya asili ya vivuli, mbao inayotumika kwa ajili ya mahtaki ua kijamii, miche rafiki kwa mazingira katika vyanzo vya maji, ambayo inazuia mmomonyoko wa udongo.

Vilevile anataja miti ya kulinda ardhi, udongo wenye rutuba, kuzalisha mbolea za shambani kwa wananchi, hivyo bustani hizo huzalisha miche ya miti milioni 2.5 kwa mwaka, ambayo hugawiwa bure mwananchi mmoja mmoja kupanda, pia taasisi za umma na zisizo za umma katika maeneo mbalimbali yaliyoathriika.

Mohamed anaeleza, ni kawaida wananchi wanahimizwa kuchukua miti ya kupanda inayoendena na mazingira yao kiikolojia, aina ya udongo, hali ya hewa katika eneo husika, iwe inayohimili mvua nyingi na ukame.

 

Pia, anasema kuwapo ufugaji nyuki uliosheheni kwenye vikundi 80, ambavyo wanavipa elimu ya ufugaji na faida za asali. Anaeleza hadi sasa, soko la asali hiyo inapatikana katika nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC).

 

Vilevile kamanda huyo wa TFS anasema, huwa wanahakikisha kuwa na mashamba mahususi iliyotengwa kwa ajili ya kupandwa anayoiita ‘miti ya kigeni’, ambazo zina uharaka wa kukidhi mahitaji mazao ya mistu, inayosaidia kuzuia uharibifu wa misitu ya asili.

Anaeleza kuwa wanayo mashamba manne yaliyohifadhiwa kwa ajili ya kuvunwa mbao, ambayo yatakidhi mahitaji ya miti katika kukuza uchumi wa nchi, mtu mmoja moja. Anayataja na wilata il;iko katika mabano. Silayo (Chato); Buhindi (Sengerema); Rubale (Ukerewe); na Rubia iliyoko Biharamulo.

Mohamed anataja maeneo yaliyopandwa miti ya kigeni kwa sasa hayazidi hekta 20,000, hivyo kila mwananchi anahamasishwa kuwa na shamba dogo la miti, itakayomnufaisha kiuchumi baadaye wakati wa kuvuna.

Shughuli zingine zinazofanywa, ni kuhudumia wafanyabisahara mazao ya misitu, wakishirikiana na halmashauri mbalimbali anazitaja ni kuhakikisha maeneo yote yanayohifadhiwa hifadhi za taifa yanalindwa, wananchi wakipewa elimu ya uendelezaji na utunzaji mazingira

CHANGAMOTO

Anasema changamoto iliyopo kwenye misitu ya asili ni uvunaji haramu, uvamizi wa mifugo kwa ajili ya malisho, akiwataka wananchi kushirikiana kufanya kazi za doria na mamlaka za wilaya husika kuwezesha kuzuia wahalifu wanaovamia maeneo hayo na kusababisha uharibifu wa misitu.

Mohamed anaeleza kuwa misitu ya asili kwa sasa ina uwezo mkubwa wa kurekebisha hali ya hewa duniani akitaja ni ufyonza hewa ya ukaa kwa kiwango kikubwa, vilevile kuhifadhi vyanzo vya maji vikiwaemo viumbe hai, akitumia mfano wa wanyama, wadudu, ndege na viumbe, vyote vikileta tija kiuchumi, kiikolojia pia kimazingira.

Anarejea kwamba madhara yanayoweza kutokea katika mistu ya asili inapovunwa holela, ni kukosekana mvua, uvuvi kuathirika, vyanzo vingi vya maji kukauka, kukumbwa na ukame, mifugo kuathirika kwa kukosa maji na malisho na hali mbaya za hewa kwa wakazi.

Kuhusu ukanda aliko, anakiri kuwapo mabadiliko ya tabianchi, ambayo yamewaathiri kiuchumi wananchi katika kilimo, uzalishaji mali na kwenue uoto wa asili kutoweka.

Rai yake Kamanda Mohamed, ni kwa viongozi wa ngazi mbalimbali za vijiji kuhakikisha wanainga mkono TFS, katika kutoa elimu ya kupiga vita uvamizi wa mistu, kwani wanafanya kazi kwa niaba yao kulinda rasilimali za nchi.

Pia, analalamika kuwapo uvamizi wa misitu kwa ajili ya kilimo, uchimbaji madini na shughuli mbalimbali za kibinadamu na mifugo, ikidhibitwa kuanzia na uelewa binafsi, itasaidia kuondoa kero ya kunyoosheana vidole.

 

 

 

Top of Form

Bottom of Form

Top of Form

Bottom of Form