Ingawa ndege nyingine zina safari hadi wastani wa saa 24, lakini abiria huunganisha kwa kutua na kupaa tena. Hapo ndipo waelewa wa taaluma hiyo, wanaitafsiri ‘ni safari inayogusa mabadiliko ya afya ya abiria.’
Pengine swali linalojitokeza, mwili unaweza kubadilikaje wakati wa kusafiri kwa muda mrefu? Ina tofauti na safari ndefu zilizopo za ndege zingine? Pata darasa:
UPUNGUFU WA MAJI
Kunatajwa kuwapo uwezekano wa upungufu wa maji mwilini kwa abiria. Abiria anashauriwa, kabla ya kupanda ndege ya safari ndefu, ahakikishe amekunywa maji ya kutosha, licha ya ukweli kwamba upungufu wa maji mwilini ni jambo la kawaida kwenye safari za ndege za masafa marefu.
Inaelezwa ndiyo maana mtu unaweza kuhisi ukavu wa koo, pua na ngozi yake kubadilika kwenye ndege. Muda mrefu wa safari unaweza kusababisha hatari kubwa ya upungufu wa maji mwilini.
Hiyo inatokana na unyevu ikilinganishwa na ule ulio ardhini. Hiyo ni kwa sababu hewa inaingia kwenye ndege kutoka nje na hakuna unyevu mwingi katika hewa ya angani.
Mtu anaweza pia kukosa maji mwilini kwa kutokunywa maji ya kutosha, au kwa kunywa pombe kupita kiasi, kwani pombe mwilini huchangia kupoteza maji mwilini. Ushauri mkubwa wa kiafya ni mtu anaposafiri anywe maji kiwango cha ziada kabla ya kupanda ndege na wakati wa kusafiri.
KUATHIRI UMAKINI
Safari inatajwa inaweza kuathiri umakini wa masikio, tumbo na usingizi hata kumwachia abiria kitendawili kama anaweza kupumzika kwenye ndege?
Kijiolojia, inaelezwa kadri panapo mgandamizo kwenye ndege unavyobadilika, hewa katika mwili wa abiria nao hubadilika na hiyo inaongezeka, kadri ndege inapopanda na mgandamizo wa hewa unapungua na kinyume chake wakati ndege inashuka, ni hali inayosababisha baadhi ya matatizo ya kawaida kama vile: Maumivu ya masikio; shinikizo kwenye ngoma za masikio wakati kuna tofauti katika shinikizo la hewa kati ya ndani na nje ya ngoma za masikio.
Pia maumivu ya kichwa hutawala kwa baadhi ya watu: Hiyo kitaalamu inatajawa kusababishwa na kutanuka hewa katika mfupa mwilini na hasa ndani ya fuvu. Vilevile, kunatajwa matatizo ya tumbo, chanzo kikuu kikitajwa zaidi ni kusumbuliwa na gesi zaidi.
Mtu anaweza kuhisi usingizi zaidi kuliko kawaida; ni hali inayosababishwa na mwili kushindwa kunyonya oksijeni nyingi kutoka kwenye ndege kama ilivyo kawaida ardhini chini.
Hali hiyo inaweza kufanya mtu ahisi usingizi, lakini ni kwamba matatizo mengi si lazima yaonekane zaidi kwenye safari ndefu za ndege, mara nyingi huonekana wakati ndege inapopanda na kushuka.
DAMU KUGANDA
Kuna changamoto ya damu kuganda na kuziba mishipa ya damu kwa safari ndefu za ndege; mara nyingi wasiwasi mkubwa kwa abiria ni eneo hilo, kutokana na kutotembea kwa muda mrefu, athari ikianzia kwenye miguu hadi kwenye mapafu.
Inatajwa kwa waliopata uzazi karibuni au baada ya upasuaji na wamekuwa wakitumia homoni au kumeza dawa za uzazi wa mpango, kadri safari ya ndege inavyoendelea, ndivyo hatari ya kuganda kwa damu zao inavyoongezeka, kulingana na utafiti uliofanyika mwaka jana.
Watafiti walihesabu kuwa hatari ya kuganda kwa damu iliongezeka kwa asilimia 26 kwa kila saa mbili za kusafiri kuanzia baada ya saa sasa nne angani.
Pia, kuna ushahidi kwamba kuvaa soksi za kubana unaweza kusaidia kuzuia kuganda kwa damu, kwani zinatajwa kuboresha mzunguko wa damu kwenye miguu na kusaidia kurudisha damu kwenye moyo.
Kwa kawaida, hiyo hutokea kutokana na kupungua kwa misuli inayosababishwa na kutembea, ukaguzi wa kisayansi mwaka juzi iliyohusisha 2,637 katika safari zikatoa majibu hayo.
Wenye kasoro za kuganda damu, wanashauriwa kupata ushauri wa kidaktari kabla ya kuruka angani.
Kwa kawaida, mtu akiwa na damu iliyoganda, inachukua muda kuzunguka mwilini ua isizungukle.
Kwa hiyo, mtu anashahuriwa kufatilia dalili zifuatazo baada ya kusafiri: Maumivu ya mguu na uvimbe (mara nyingi mguu mmoja tu), maumivu ya kifua, kikohozi na upungufu wa pumzi na kupata usaidizi wa dharura wa matibabu ikihitajika.
ATHARI ZA MIONZI
Inatajwa hyaijalishi kwenye eneo lipi la abiria wa ndege, lazima asimame na atembee kila mara. Ikiwa inaruka umbali mrefu mara kila mara, inatajwa abiria anavyokaa muda mrefu angani, pia anapata zaidi mionzi ya anga.
Inatajwa mionzi kutoka angani, inaweza kuongeza saratani na hasa za uzazi, kwani haijulikani ni mionzi ipo iliyo salama. Ushauri ni kwa mjamzito ni bora kushauriana na daktari wake kabla ya kuruka angani.
Kimsingi, baadhi ya tahadhari za kawaida zinahitajika kuchukuliwa, kama vile kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa na kutosafiri ikiwa unajisikia vibaya.
Kwa kifupi, utafiti kuhusu mwili wa binadamu unavyoweza kuguswa na safari ndefu za ndege za moja kwa moja kati ya Australia na Ulaya, bado uko katika hatua zake za awali na timu ya Australia kwa sasa inashughulikia hilo.
Hadi matokeo yawepo, ushauri wa kushughulika na safari za ndege za masafa marefu zitatangazwa. Kwa sasa abiria wanapaswa kufuata vidokezo vya shirika la ndege kama vile kumuona daktari kabla ya kusafiri, pia kunywa maji mengi, kuvaa barakoa na kudumisha tabia ya usafi, kunawa mikono kila mara.
Abiria anashauriwa kufuta matibabu ya haraka ikiwa atapata dalili zozote za kutisha baada ya safari ya ndege.









