Kimsingi, inabeba kama walivyo wachambuzi na wataalamu wote wa sayansi ya siasa, wanajikita katika uhalisia wa siasa, pia nafsi yake binafsi mkuu huyo.
Rais Dk. Samia leo akitumikia nafasi hiyo ofisi yake ikiwa upande wa bara, mzizi wake ni mzaliwa wa Visiwani Zanzibar, alikosoma shule hadi kufunga ndoa yake. Hata hivyo, alivyojiunga na ngazi ya chuo, akaangukia kunufaika na duru za Muungano walizoanzisha watangulizi wake wastani muongo mmoja kabla, akijiunga na Chuo cha Uongozi wa Maendeleo (IDM) - Mzumbe, vilevile Chuo Kikuu Huria (OUT), miaka nane iliyopita.
Ukirejewa mzizi wa uzoefu wa ajira yake hadi kujitosa siasa, Dk. Samia ameipatia Zanzibar, hususan Unguja alikozaliwa, akachipua kuanzia mwaka 2,000 alipojiunga rasmi kwenye siasa hai, akigombea ubunge wa viti maalum kwa bendera ya CCM na akaipata nafasi hiyo.
Hapo akamea zaidi kisiasa, pale Rais wa Zanzibar wakati huo, Amani Abeid Karume, alipomteua kuwa Waziri wa Utalii na Biashara, katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Akarejea tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, akachaguliwa tena kwenye viti maalum na ilipoundwa Baraza Mawaziri, yeye akakabidhiwa Wizara ya Kazi, Jinsia na Watoto ndani ya SMZ. Hadi kufika mwaka 2010, Samia alikuwa na uzoefu wa kutosha miaka 10 katika siasa na nafasi hizo.
Hapo Mama Samia, katika kile kiliendana na wito uliokwishatolewa awali ndani ya CCM huko nyuma kwamba kinamama wanaopitia viti maalum, ni vema wakafanya maboresho wakijitosa kuwania viti majimboni, naye akafanya hivyo kupitia jimbo la Makunduchi Unguja, akatwaa nafasi, safari hiyo ikiwa ni ya Bunge la Muungano.
Kwenye matokero hayo, jimbo la Makunduchi na akafanikiwa kupata ushindi wa kishindo wastani wa asilimia 80, ukimpa jukumu la kuvuka bahari kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge Tanzania Bara, jijini Dodoma, nyum aya pazi akiwa na uzoefu wa kutosha kuwajibikia wizara za kibishara, utalii, jinsia, kinamama, watoto na ajira.
Rais Jakaya Kikwete, wakati huo akiwa katika awamu ya pili ya uongozi wake, akavutiwa naye, hata kumuweka kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulilikia Muungano. Hapo nako kukawa wigo uliotamnua zaidi na mambio yanahusu Muugano, hata Mazingira.
Ilipofika mwaka 2014 kuibuka Bunge Maalum la Katiba, Dk. Samia aloshaiva mno hata akakasimiwa kuwa Makamu Mwenyekiti, ikiwa lina na sura ya Muungano, kukitawaliwa mjadala wa dai la katiba mpya ya nchi, jambo ambalo hadi sasa halijamtoka ‘mkononi’ kukisikia michakato mbalimbali anayoenda nayo hadi leo.
Sura moja ya utekekezaji wake inashuhudiwa hivi karibuni, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro, akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini hapa, akasema mchakato wa Katiba mpya unatarajiwa kuanza kufanyiwa kazi baada ya kupitishwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Historia ya heshima na neema ya kiuongozi katika picha ya Muungano, ikaendelea kudumu kwa Dk. Samia alipopanda daraja daraja kuteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Dk. John Magufuli, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na hata baada ya ushindi, akawa rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Kimsingi, alipanda daraja katika ofisi aliyotumikia akiwa waziri, wajibu mpya akiwa mwelekezaji na msimamizi mkuu wa masuala ya Muungano na Mazingira, pia Msaidizi Mkuu wa Rais, alikodumu kwa muhula na hata baada ya uchaguzi uliofuata mwaka 2020, akabaki kwenye nafasi hiyo kwa wastani wa mwaka mmoja, hadi kilipotokea kifo cha Rais Dk. Magufuli, akakasimiwa urais kwa mujibu wa katiba.
Hadi kufika Aprili 30 2021, akawa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama tawala - CCM, katika ukanda wote wa Muungano.
Mbali na kutumikia nafasi hiyo ya juu, kusimamia mihimili ya Muungano kwa chama tawala, hadi serikali, katika familia yake ameunda zao la kuwa na binti, anayechipukia kwa njia zake, akiwa Mbunge wa Viti Maalum ndani a Bunge la Jamhuri ya Muungano.
HISTORIA YA NCHI
Rais Dk. Samia katika historia ya nchi, ana jingine kwamba ni rais wa pili kutoka upande wa Zanzibar, tangu kupatikana Muungano mwaka 1964, akitanguliwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliyestaafu miaka 26 kabla ya urais wake, 1995.
Kingine cha kihistoria kitaifa na kimataifa kuanzia na ulingo wa Muungano, Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata anga za mbali akaonyesha kuwa “Rais mwanamama anayeweza kwa vitendo akiweka rekodi ya kazi kadhaa kimataifa ndani ya miaka mwili,” ikiwa na mrejesho wa sifa za Muungano.
Leo hii, Rais Dk. Samia katika sura nyingine ana zawadi kubwa ya kijinsia anakionyesha kutetea kinamama katika timu ya Muungano, kuanzia safu yake ya Baraza la Mawaziri ikisheheni timu ya ‘kinamama wanaoweza’, hadi nyenzo za wateule wake wanaongoza mikoa na wilaya wakishamiri kinamama, pia historia kwa baadhi ya wizara kama Ulinzi, kwa mara ya kwanza kuongozwa na mwanamama.
Hilo linaendana kutosahau kada ya vijana, ambayo alitangaza wazo kwamba ndio anawapa nafasi hata katika upande wa timu ya Baraza la Mawaziri.










