Hata katika hospitali ta Rufani ya mkoa wa Pwani ya Tumbi, inajulikana kuwa sehemu kubwa ya wagonjwa wake ni wanaotokana na ajali za barabarani.
Sababu kuu ni kwamba Kibaha, kunapitiwa na Barabara Kuu kati ya Dar es Salaam na Morogoro na iendayo Moshi.
Miaka iliyopita, kulishawahi kutokea ajali mbaya iliyosambaratisha uhai wa askari wawili wa usalama barabarani wakiwa kazini na mmoja akiwa mahututi.
Kwa ujumla, hali mbaya ya ukiukwaji wa uendeshaji barabarani, umewaweka madereva wa eneo hilo kuwa na wakati mgumu.
Hadi sasa taarifa za Usalama Barabarani mkoa wa Pwani, zinaeleza kuwa askari walioukufa kwa ajali kazini, hadi kipindi cha mwaka 2014/2016 inafikia 13.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Boneventure Mushongi anasema katika cha karibuni askari watano wamefariki katika ajali za barabarani, wawili kati yao waligongwa wakiwa wanaongoza magari barabarani.
Anasema wengine waliuawa na majambazi wakiwa kazini katika vituo vyao vya kazi.
Katika mfululizo wa matukuo hayo, hivi karibuni askari wa ysaklama barabarani, Joseph Mchiwa (37), alifariki saa tatu usiku, baada ya kugongwa na gari akiwa anaongoza magari.
Ni tukio lililotokea Aprili 24 mwaka huu katika eneo la Kwa Mbonde, Kibaha katika Barabara Kuu ya Morogoro.
Kamanda Mushongi anakiri marehemu alikuwa mchapakazi na anaongeza: “PC (Konstebo) Mchiwa alikuwa mtendaji mzuri. Kifo chake kimeacha pengo kubwa, kwani alikuwa mtu anayejituma na anayependa kazi yake.”
Kamanda Mushongi anafafanua kuwa kifo chake kilisababishwa na uvunjifu wa sheria za barabarani, kwa dereva wa lori alijaribu kupita magari mengine, ndipo alipomgonga marehemu aliyekuiwa akiongoza magari.
Kutokana na hilo, anatoa wito kwa madereva kufuata sheria za barabarani na kwa upande wa askari wa usalama bararani, amewataka kuvaa koti zenye alama za barabarani (reflector) na vifaa vingine vinavyotumika usiku, kuwasaidia waonekane kwa madereva haraka.
“Wito wangu kwa askari ni kuwa makini wanapokuwa barabarani. Nawakumbushaa kutumia vifaa vinavyowatumbulisha kwa haraka.
“Gari ni mashine, wakati wowote laweza kukosa breki, haliwezi kutambua huyu ni trafiki lisimgonge, kile ni chombo na hata madereva nao wanapaswa kuwa waangalifu wawapo barabarani.
Endapo watafuata sheria za usalama barabarani, tutaweza kuepuka ajali hizi zinazosababishwa na uzembe”, anasema Kamanda Mushongi.










