Kuna shinikizo kubwa kwao wanapopeleka vikundi vyao vya wanasoka wenye vipaji vya hali ya juu kwenye tukio la maonyesho ya mchezo huo maridadi. Kazi ya makocha wa timu ya taifa si rahisi.
Kuna majina mengi yanayotambulika katika mzunguko wa kufundisha siku hizi, litakuwa jambo la kuvutia kuona ni nani anayebeba fedha nyingi nyumbani. Makala haya yanawaangalia makocha watano wanaolipwa pesa nyingi zaidi kuelekea katika Kombe la Dunia la FIFA la 2022, twende sasa...
#5. Louis van Gaal (Uholanzi) - Pauni milioni 2.5 kwa mwaka
Louis van Gaal amekuwa na kazi nzuri ya ukocha. Ana umri wa miaka 71 sasa, na hili litakuwa Kombe la Dunia la mwisho kwa kocha huyo wa zamani wa Manchester United na Barcelona.
Van Gaal amefanikiwa kufanya kazi nzuri akiwa na Timu ya Taifa ya Uholanzi tangu alipostaafu kuinoa Agosti 2021. Alichukua nafasi hiyo baada ya Frank de Boer kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya timu kwenye michuano ya Euro 2020.
Van Gaal ndiye kocha wa tano wa timu ya taifa anayelipwa zaidi duniani kwa sasa na anapokea pauni milioni 2.5 kwa mwaka.
#4. Tite (Brazil) - Pauni milioni 3 kwa mwaka
Tite amekuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Brazil tangu mwaka 2016. Aliiongoza kutwaa ubingwa wa Copa America mwaka 2019, na tayari amefichua kuwa ana nia ya kujiuzulu kama kocha wa 'Selecao' hao baada ya michuano hii ya Kombe la Dunia.
Kwa hiyo Kombe la Dunia la 2022 litakuwa la mwisho kwa Tite akiwa na timu hii ya Brazil yenye vipaji vingi. Tite amefanya kazi nzuri sana akiwa na Brazil katika miaka ya hivi karibuni na timu yake haikufungwa kwenye mechi za Kufuzu Kombe la Dunia kwa ukanda wa Amerika Kusini.
Tite ni mmoja wa makocha wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani akiwa anapokea pauni milioni tatu kila mwaka.
#3. Didier Deschamps (Ufaransa) - Pauni milioni 3.2 kwa mwaka
Didier Deschamps aliiongoza Ufaransa kutwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 2018. Walipewa nafasi kubwa ya kushinda Euro 2020 pia, lakini timu hiyo ilitolewa katika hatua ya 16-bora.
Deschamps huenda akalazimika kuwa bila nyota wake wa kati wawili, N'Golo Kante na Paul Pogba kwa kuwa hao kwa sasa ni majeruhi. Wengi wa washindi wake wa Kombe la Dunia pia wamepitwa kiwango chao. Lakini hiyo haimaanishi kuwa kuna uhaba wa vipaji au ubora katika upande wa Ufaransa.
Mshahara wa Deschamps wa kila mwaka ni pauni milioni 3.2 na hiyo inamfanya kuwa kocha wa tatu anayelipwa zaidi katika Kombe la Dunia 2022.
#2. Gareth Southgate (England) - Pauni milioni 4.9 kwa mwaka
Gareth Southgate amefanya kazi nzuri akiwa na Timu ya Taifa ya England. Licha ya hali yao ya sasa, England ilitinga nusu fainali ya Kombe la Dunia la 2018.
England kwa sasa ina kikosi chenye vipaji vya hali ya juu na chenye nyota wengi na wanaweza kucheza soka la kusisimua zaidi.
Southgate anapokea mashahara wa pauni milioni 4.9 kwa mwaka.
#1. Hansi Flick (Ujerumani) - Pauni milioni 5.5 kwa mwaka
Hansi Flick alishinda mataji matatu akiwa na Bayern Munich msimu wa 2019-20. Kisha akachukua jukumu la kuinoa Timu ya Taifa ya Ujerumani ambayo imekuwa ikipitia nyakati ngumu hivi karibuni. Aliiongoza bila kufungwa katika mechi zake 10 za kwanza akiinoa Ujerumani.
Ujerumani ilitinga hatua ya makundi katika Kombe la Dunia 2018 na kuna shinikizo kubwa kwa Flick kubadili mambo wakati huu. Flick anaingiza pauni milioni 5.5 kwa mwaka kama kocha wa Timu ya Taifa ya Ujerumani na ndiye kocha anayelipwa fedha nyingi zaidi katika Kombe la Dunia la 2022.










