Sura ya huduma hizo zinajumuisha elimu, afya, makazi na nyenzo bora zinazowezesha roho ya nchi kiuchumi, sekta ya kilimo. Hilo katika awamu zote sita za uongozi nchini, hazijawahi kuachwa, bali zinabadilika kulingana na mahitaji ya wakati.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan naye katika zama zake madarakani, akiwa na sura ya maboresho ya ubunifu wake, anaendeleza, ikiwamo katika sekta yake kipenzi - elimu, ambako yu muumini hasa.
Hiyo inashuhudiwa hata na watendaji wake wateule, akiwamo Kanali Wilson Sakulo, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, katika ufunguzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Omom Preci iliyopo Loliondo, anapowaasa wananchi kijijini na kata ya Enguserosambu, kuhakikisha hawakai mbali na sera, pia falsafa ya Ukombozi wa Elimu kwa kila Mtanzania.
Msaidizi huyo wa Rais Nambari Moja, wilayani hapo, anawakilisha wasifu wake kuwa sauti na kioo cha serikali kinachosisitiza elimu kwa wote.
Katika hafla hiyo hivi karibuni, kamanda huyo anaawaambia umati wilayani kwake kuwa, Rais Dk. Samia na serikali ya Awamu ya Sita tangu alipochukua Madaraka, vitendo na maneno yake vimeonakana kuhimzia elimu.
Hivyo, Kanali Sakulo anawataka wananchi hao kutokuwa na visingizio mbadala dhidi ya ‘elimu bure shuleni’ kwa watoto wao, utekelezaji wake ukifikishwa kwa kila mwananchi alipo nchini.
Kimsingi, kwa miaka mitatu, Rais Dk. Samia tangu ashike madaraka Machi mwaka 2021, amedumu kuwa muumini wa kupatikana elimu kwa watoto wote wa Kitanzania, akikataa mzaha dhodi yake.
Huo umedumu kuwa mwelekeo na falsafa inayoendelezwa na wasaidizi wake kikazi, kwa ngazi mbalimbali kama vile; Wakurugenzi wa Halmashauri (DED s), maofisa wanaowasaidia, pia watunga sera za elimu ngazi mbalimbali, wakizama katika imani na itifaki hizo kikazi, ambayo pia ndio uhai wa nchi.
Eneo moja la mfano katika hatua zake Rais Dk. Samia, akaanza kutumikia wajibu wa ukuu wa nchi kama mama mwaka 2021, kwa kuwarudisha shuleni wanafunzi wanaopata mimba.
Hapo ndipo Mkuu wa Wilaya Kanali Sakulo, akiwaambia wananchi wake kuwa hakuna kisingizio chochote kukaa mbali na shule katika Serikali ya Awamu ya Sita.
Kihistoria, elimu ni kigezo muhimu sana katka kuleta maendeleo ya nchi, hivyo serikali zianwajibibika kuwasimamia na kuwanasua wanapokwama katika safari ya raia kuelekea kuelimika.
Ndipo kunashuhudiwa udhamini wa serikali masomoni na sheria chanya, kusaidia wanaosoma. Itakumbukwa ndilo alilifanya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, mara tu alipokabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi, baada ya uhuru.
Suala la elimu nchini linasisitizwa kila mara na kila, mahali kifalsafa na kimatendo ikiendelezwa sasa serikalini katika staili hata aliyeachwa nyuma anakokotwa kufika safari.
Nchini kuna matukio ya mazoea na mila, baadhi ya wana wanafunzi kuozeshwa au kuolewa kutokana na kukosa nafasi ya pili ya kurekebisha makosa yao.
Hapo ndipo Serikali ya Awamu ya Sita, inatumia kigezo maendeleo, ikitumia elimu kuwa ‘ufunguo wa maisha’ kwa wahusika, mahsusi kwa watoto wa Kitanzania.
Inafahamika, maeneo ya mijini na vijijini, kunawanafunzi wanaopata mimba za utotoni. Pasipo kujali takwimu, suala la mimba hizo limekuwa nyeti, kwani linadhoofisha maendeleo ya watoto husika.
Kwa kutambua kuwa taifa linaweza kuangamia kwa kuruhusu wanafunzi waliopata mimba, wakikosa fursa za elimu tena, serikali sasa imekuja na mpango unaonufaisha wananchi na kuwaondolea kero ya kukoda elimu.
Pili, kinachoshudiwa, Rais Dk. Samia amefanya ubinfu, akituimia pia wahisani kupata mikopo na ufadhili za kuzibna mapengo kwenye uwezeshaji sekta elimu.
Miongoni mwa miradi iliyookoa sekta ya elimu ni pamoja na ufadhili wa fedha za kufharamia tiba Uviko 19, sasa zikahamishiwa kujenga vyumba vya madarasa sehemu mbalimbali nchini.
Katika marejeo ya suala la ujenzi wa vyumba vya madarasa, limepata kukumbushwa pia wakati wa uzinduzi wa Omom Preci inayofadhiliwa na Shirika la Tanzania Heritage Foundation, ambako Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, anayesisitiza wananchi kupewa nafasi ya kupata elimu kutoka kwa watu binafsi na serikalini.
Hapo, wananchi wanatakiwa kutumia fursa hizo, kwani serikali inawapa nafasi wadau kuchangia.
Fedha hizo pia zilitumika kutengeneza madawati ambayo yamekuwa msaada kwa wanafunzi na kutatua kero yao sehemu mbalimbali.
Ni aina ya juhudi zinazoifanya serikali ya sasa, kubeba sifa za ukombozi thabiti wa elimu na kupigania ustawi wa jamii, katika safari ya kuyasaka maendeleo.
Lingine linalotajwa, linasimama katika kinachohimizwa na Rais, mkakati wa serikali kumiliki shule za msingi na sekondari zenye mkondo wa lugha ya Kiingereza.
Tayari zipo shule za serikali zinafundisha kwa kutumia mkondo wa lugha ya Kiingereza na kuwapo mtaala mpya unaokaribisha somo la Kichina, ambalo sasa ni sehemu ya stadi za Uchumi na maendeleo ya dunia.
Hiyo pia, ni mustakabali unaowapa nafasi wadau binafsi na watumishi watoto wao wanapata elimu sahihi, vilevile katika sura ya pili taifa nalo likijiboresha mahitaji yake kitaifa na kimataifa kwa; biashara, kiuchumi, kijamii na mawasiliano.
Hapo napo panapandisha thamani ya shule za serikali na elimu ya nchj kimataifa, kukiwekwa jicho kali elimu bora kuwa na sura endelevu.
Hapana shaka, wakati serikali ya Awamu ay Sita, moja ya mitaji yake ya mipango elimu, kunashuhudiwa sekta ya elimu ambako hata ngazi ya juu vyuoni, kumekuwapo maboresho ya mikopo hadfi ngazi za chini, upendeleo wa kijinsia, udhamini wa masomo.
Pia, wiki hii kumetangazwa mwelekeo ya kusuka upya mtaala wa Shule ya Sheria, inayozalisha watalamau wa mahakamani, ambako ni nguzi kuu ya dola, sambamba na bunge, pia serikali.










