Kila baada ya muda, amekuwa akizunguka kimataifa akinadi uchumi wa nchi kimataifa, hali kadhalika akifungua soko la yapatikanayo nchini.
Hapo Rais Dk Samia ana sura kuu tatu; kuuza bidhaa na huduma nyingi nchini, zikiwamo kilimo na utalii; kukaribisha wawekezaji nchini katika sekta mbalimbali; na zao la yote inafungua wigo mpana wa ajira kitaifa.
Inaporejewa dhana pana ya diplomasia uchumi ambako Rais Dk. Samia ni muumini wake mkubwa, ina mzizi katika Sera ya Taifa ya Mambo ya Nje, toleo la mwaka 2001, inayobeba tafsiri ya dhana ya “diplomasia ya uchumi.”
Hapo inataja, mbali na malengo yake ya msingi kama vile kiulinzi, pia inajikita katika kujenga na kuimarisha uchumi wetu, inaushukilia uchumi wa nchi kiamtaifa, kwa wigo wa msimamo nchini.
Utekelezaji wa sera hiyo unaanzia katika kuimarisha misingi na umuhimu wa sera za asili za nchi, huku ikiongozwa na kanuni kadhaa, ikiwamo ya kulinda uhuru wa taifa, haki za binadamu, na usawa na demokrasia.
Kuna mengi yanaangukia zao la sura hiyo, ikiwamo kumkaribisha nchini Rais wa Romania, Klaus Iohannis, ambayo nayo ikajenga historia, kwamba kiongozi wa juu wa taifa hilo kutembelea Tanzania, hata ikasaidia kuimarisha ushirikiano katika maeneno ya kimkakati.
Rais Iohannis alifanya ziara ya kwanza ya siku nne na akaeleza kuwa, katika mazungumzo na mgeni wake walikubaliana kuwa mataifa yatakayoimarisha ushirikiano katika sekta za afya, hususan utengenezaji dawa, usindikaji mazao ya kilimo, madini na mbinu za kukabiliana na majanga.
Maeneo mengine ya ushirikiano ambayo viongozi hao wakadhamiria kuyapa kipaumbele, ni ufadhili wa masomo ambao Romania ikatoa nafasi 10 kwa ajili ya Watanzania kusoma masomo ya udaktari na ufamasia katika mwaka wa masomo uliopo.
Hapo, Tanzania nayo ikatoa nafasi tano za masomo kwa wanafunzi wa Romania kuja nchini katika vyuo watakavyochagua wenyewe, huku Dk. Samia akitangaza kudhamiria kukuza kiwango cha biashara na uwekezaji, nchini.
Rais wa Romania, Klaus Iohannis alikutana na kuzungumza na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi., aliyezikaribisha kampuni za Romania kuwekeza Zanzibar katika sekta za Uchumi wa Buluu na Utalii, ambazo ni sekta za kipaumbele huko Visiwani.
Hapo Rais Iohannis, akaeleza kufurahishwa na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar, akimuahidi Dk. Mwinyi, atashirikiana na Zanzibar kufanikisha utekelezaji wa dira hiyo.
Akasema ziara yake ni moja ya jitihada za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kati ya Romania na Tanzania, ambayo mwezi Mei 2024 utafikisha miaka 60 tangu ulipoanzishwa mwaka 1964.
Hadi sasa, Romania imeshaahidi kuisaidia Tanzania katika usindikaji wa mazao ya kilimo, nchini kukinufaika na teknolojia za kisasa ikisindika mazao ya kilimo na kuuza bidhaa nje badala ya malighafi, hata kimasoko inafungulia uingizwaji fedha za kigeni nchini kwa wingi.
Hati zilizotiwa saini Novemba 17, 2023 jijini Dar es Salaam, zikahusu ushirikiano wa kiuchumi, kisayansi na kiufundi katika sekta za kilimo na mazingira.
Mwanzoni mwa mwaka huo, mwezi Machi katika sura ya ushirikiano na taifa la India, ilifungua wigo kufanyika biashara ya mabadilishano yenye thamani ya shilingi trilioni 10.4.
Hapo ikawa ni kuingiza nchini bidhaa za India thamani ya shilingi trilioni 5.3 na Watanzania nao wakiuza nje bidhaa zenye thamani ya shilingi trilioni 5.1.
Kilicholeta mvuto mkubwa kitaifa ni namna biashara hiyo ikaafikiwa kufanyika, ambayo badala ya kutumika Dola za Marekani, sasa inatumika shilingi za nchini na Rupia ya India.










