Waliosababisha kifo cha Mohbad waanza kushikwa

02Oct 2023
Nipashe
Waliosababisha kifo cha Mohbad waanza kushikwa

JESHI la Polisi nchini Nigeria limethibitisha kumkamata Balogun Olamilekan Eletu, maarufu kama Sam Larry, kwa kuhusika na kifo cha mwanamuziki Ilerioluwa Aloba, aliyejulikana kwa jina la Mohbad.

Mohbad.

Sam Larry ambaye anatoka lebo ya muziki ya Naira Maeley, amekamatwa katika uchunguzi unaoendelea kuwabaini watu waliohusika na kifo chake.

Msemaji wa Polisi, SP Benjamin Hundeyin, aliandika kwenye mtandao wa X kuwa Balogun Olamilekan Eletu yuko chini ya ulinzi wao kuanzia jana.

 “Kwa sasa anasaidia uchunguzi unaoendelea.” amesema

Tayari bosi wa lebo hiyo ya Marlian Record, Naira Marley, amedai kuwa anafanya mipango ya kurejea Nigeria kuheshimu wito wa polisi kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusu kifo hicho.

Mohbad alikufa katika mazingira ya kutatanisha mnamo Septemba 12, mwaka huu.

Katika video ambayo ilisambaa mitandaoni baada ya kifo cha mwimbaji huyo, Sam Larry alionekana akivamia kundi la muziki na kumtishia Mohbad akiwa na watu wenye silaha.