Jumla ya wasanii 200 kutoka mataifa mbalimbali duniani watashiriki kwenye tamasha hilo, kati ya hao 150 ni watapanda jukwaani kutoa burudani ya muziki wa aina mbalimbali.
Uzinduzi huo ulianza kwa kufanyika kwa gwaride maalum kutoka ofisi ya Taasisi ya ASADEVA ambayo ni mwandaaji hadi katika viwanja vya makumbusho.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa taasisi ya Asedeva, Isack Abeneke amewataka watanzania kwenda kufurahia burudani halisi yenye mchanganyiko wa tamaduni kutoka nchi tofauti.
Amesema tamasha hilo litadumu kwa muda wa siku tano katika miji miwili ya Dar es salaam na Bagamoyo.
“Majukwaa mawili ya muziki yenye hadhji ya kimataifa yatatumika kutoa burudani, moja litakuwa Makumbusho mkoani Dar es salam kwa siku tatu na Bagamoyo mkoani Pwani kwa siku moja, nawakaribisha mashabiki wote wa musiku kuja kuburudika live,” alisema Abebeke.
Licha ya burudani, pia kuna maonyesho ya sanaa ya mikono, vyakula na mafunzo kwa wanamuziki namna ya kutumia mitandao kujinufaisha kiuchumi na kufahamu umhimu wa hakimiliki ya kazi zao.









