Wakali wa Muziki Afrika Mashariki watikisa Tamasha la Serengeti Lite

23Oct 2023
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Wakali wa Muziki Afrika Mashariki watikisa Tamasha la Serengeti Lite

WASANII wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Kenya na Uganda wamekutana kwenye jukwaa moja na kushusha burudani katika Tamasha la Utamaduni, muziki na utamaduni wa kiafrika la Serengeti Lite Oktobafest.

Tamasha hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika fukwe za Coco na kuudhuriwa wapenda burudani kutoka afrika mashariki.Wasanii hao ni Nyamari Ongegu maarufu Nyanshiski kutoka Kenya, Jose Chameleon kutoka Uganda, Ali Kiba, Bill Nas, Chino, G Nako, kutoka Tanzania pamoja na wabunifu kama vile Makeke International kutoka Tanzania.

Meneja wa Chapa kwa Serengeti Lite na Serengeti Premium Lager, Esther Raphael, alisema maadhimisho ya tamasha hilo la muziki na utamaduni ni jukwaa lililowezesha vijana wa Afrika Mashariki kupata fursa za biashara kupitia burudani na ubunifu mbalimbali.

"Zaidi ya hayo, tamasha hili linaonyesha jinsi bia inaweza kutumika kama daraja, kuwaunganisha tamaduni na watu mbalimbali wa Afrika Mashariki kwa lugha ya muziki," alisema

Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu,Rispa Hatibu alisema fahari la tamasha hilo pia ni kuzingatia utunzaji wa mazingira. 

"Serengeti Lite Oktobafest ilikuwa tamasha lenye kutunza mazingira bila taka zozote, ambapo mazingira yalipewa kipaumbele.Timu yetu ya waokota taka ilifanya  kazi kwa bidii kuhakikisha mazingira safi ni kila wakati wakati wa tamasha katika fukwe za coco," alisema