Katika mahojiano na kituo cha radio cha East Africa, Mwana FA alisema kuwa wasanii wanataka kufanya vitu ambavyo hawana uhakika navyo hata kama vinaingiza fedha nyingi.
"Muziki umebadilika sana, umetoka katika ile misingi iliyowekwa na sababu zake za kuwapo, umekuwa starehe na hela peke yake. Yaani ile misingi imebadilika sana, na vitu vingi ambavyo vilikuwa vinapingwa vilionekana vya kipumbavu mwanzoni huko, sasa hivi ndio kama mtindo, watu wanafanya watakavyo kwa sababu wanataka kutengeneza pesa tu.
Muziki umekuwa biashara kiukweli, kama unaleta hela kwa nini watu wachukie hela zao, lakini ninachopinga ni kuipoteza kabisa misingi ya Hip Hop kwa sababu ya hela.
Kuna vitu vingi vya kufanya na bado ukapata mkate wako wa kila siku, sio lazima usingizie unafanya aina hii ya muziki tunayoifanya wakati huna kipaji nayo, hivyo ni lazima kujisingizia kufanya kitu usicho na uwezo nacho ili tu uingize hela," aliongeza msanii huyo.










