Amini: Niko fiti katika kazi

15Feb 2016
Sabato Kasika
Nipashe
Amini: Niko fiti katika kazi

BAADHI ya watu wamekuwa wakiamini kwamba wasanii wanapoingia kwenye ndoa hata uwezo wao wa kufanya kazi huwa unashuka kutokana na majukumu yanayokabili.

AMINI NA LINAH

Miongoni mwa wale ambao wanadaiwa kushindwa kufanya kazi ya muziki kikamilifu ni msanii Marlow ambaye baada ya kufunga ndoa na msanii mwenzake Besta amekuwa hasikiki kama zamani.

Hata hivyo, suala la kuoa sio shida kwa nyota wa muziki wa kizazi kipya, Amini Mwinyimkuu ambaye anasema kuwa haamini suala la kuoa linachangia kushusha kiwango cha muziki cha msanii.

"Unajua kila mtu ana mtazamo wake, wengi wanasema hivyo kuwa msanii ukioa unashuka, mimi ninakataa kwani kwa upande wangu mke amekuwa akinisaidia sana na kunishauri hasa katika suala la uandishi wa nyimbo," alisema Amini.

Alisema kuwa huo ni mtazamo wa wasanii wachache na kuongeza kwamba yeye amekaa kimya kwa kupisha kazi za wenzake zilizoingia sokoni ziwezi kutambulika na muda muafaka utakapofika naye atatambulisha nyimbo zake mpya.

Amini kwa sasa ana mke baada ya kufunga na msanii mwenzake wa muziki wa huo, Farida aliyeimba wimbo wa 'Kantangaze'.