Msanii huyo amesema kuwa wasanii wa kike wanatakiwa kujua wamefuata nini kwenye muziki na kuacha kupapatikia mambo makubwa, ambayo yanaweza kuwaharibia malengo yao ya baadaye.
"Mimi ninafikiri kwanza watoto wa kike wajue wamefuata nini kwenye muziki, ninasema hivyo kwa sababu hii sanaa ni pana sana na ina watu tofauti na katika mazingira hayo siyo kila mtu ni mwema," amesema Mwasiti.
Amesema kinachotakiwa ni wasanii wenyewe kuwa makini na kuzingatia kile ambacho kimewaingiza kwenye muziki huo, vinginevyo wanaweza kujikuta wakiingia kwenye midomo ya mamba.










