Amesema kuwa wasanii wa Bongo anawaogopa kwa sababu ni pasua kichwa, wakati yeye ana wivu wa kupindukia ambao unaweza kumfanya akonde, hivyo ni bora ajiweke pembeni.
"Mimi nina wivu sana, mazingira ambayo tuko nayo nadhani nitakonda mara mia, ndiyo maana nimeamua kwamba nisitoke na msanii wa Bongo kwani ninajua wengi wao wana mambo mengi," amesema Dayna na kuendelea:
“Sijawahi kufikiria kuwa na uhusiano na wasanii kwa sababu nawaogopa, ni pasua kichwa kwani kama nilivyosema, mimi nina wivu sana, hivyo ninaogopa kuumizwa."









