Snura ageukia ngoma za asili

29Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Snura ageukia ngoma za asili

MSANII wa Bongofleva na muigizaji wa filamu, Snura Mushi amesema kuwa ataanza kuchanganya ngoma za kwao katika muziki wake lengo kubwa likiwa ni kujiongezea mashabiki zaidi.

Msanii Snura Mushi

Snura alisema kuwa anapokuwa jukwaani huwa hana mchezo na amekuwa akiwachangamsha mashabiki wake kwa kucheza kila aina ya mtindo wa kisasa, lakini ameona kuna haja ya kuongeza vionjo vya asili.

"Binafsi huwa kuacha kucheza jukwaani ili kulinda heshima yangu mbele ya watoto wadogo, lakini ninashindwa kutokana na kuwazoesha mashabiki wangu," alisema.

"Nahitaji fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya familia, ndio maana nimeamua kuongeza ubunifu kwenye muziki wangu ili kuwavutia mashabiki wangu."