Nature: Ninaheshimu sana mashabiki

19Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Nature: Ninaheshimu sana mashabiki

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature amesema jina lake limendelea kwa vile anajiheshimu na pia anaheshimu mashabiki wake ambao ndio wateja wakubwa wa kazi zake.

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature

Alisema katika maisha yake hawezi kudharau shabiki kwa vile, anatambua nafasi yako katika sanaa ya muziki.

"Hao ndio wamenifanya nisishuke kimuziki, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa nimeshuka na hata kufikia kutofanya kazi na mimi, lakini ukweli ni kwamba niko fiti," alisema na kuongeza:

"Mimi ninajiamini na siwezi kushuka kimuziki, ndio maana niliwahi kufanya tamasha kubwa la kutumiza miaka 16 kwenye fani. Mimi ni bidhaa tayari, tena yenye ubora ni kama gari aina ya Benz."