Ushauri huo ulitolewa na wa muziki wa kizazi kipya na filamu Baby Madaha na kufafanua kuwa wakizingatia hilo watafanikiwa.
Alisema mafanikio yametokana na kujituma na kuandaa kazi zenye ubora unaokubalika.
"Ndio maana ninawashauri wasanii wenzangu wajitume ili wafikie malengo waliojiwekea kama mimi ambaye sasa niko mbioni kuzindua kampuni yangu," alisema.
Alisema yeye kama msanii hana budi kuwashauri wenzake na hasa wa kike ili waige mfano huo kama wanataka kupiga hatua zaidi, badala ya kuridhika na umaarufu tu.
"Huo ni ushauri wa bure kwa wenzangu wanaotaka kufanikiwa katika sanaa. Mimi ni miongoni mwa wasanii waliopiga hatua, hivyo lazima niwashauri wenzangu pia," alisema Madaha.
Alisema kwa sasa yuko mbioni kuhamia Dubai kufanya shughuli za muziki, huku kampuni yake nayo ikiendelea na kazi nchini.
Mbali na muziki wa kizazi kipya, msanii huyo amekuwa akitamba na filamu mbalimbali, ikiwamo ya 'Saint & Ghost' ambayo ameiandaa kwa lengo la kuiingiza kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za kimataifa.










