Tamasha hilo lenye kaulimbiu ya 'Tupo Veree', linatarajiwa kufanyika Julai 23, mwaka huu, katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma likishirikisha wasanii wengi wa ndani na wengine kutoka nje ya nchi.
Wiki iliyopita, msanii huyo alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa anasubiri kwanza afunge ndoa ndipo aweke hadharani majina ya wasanii hao.
Tayari ameshafunga ndoa na msanii mwenzake Billnass na sasa kilichobaki ni kutangaza majina ya wasanii hao watakaosaidia kufanikisha tamasha hilo ambalo safari hii atalifanya akiwa ni mke wa mtu.
Nandy alikaririwa akisema kuwa pamoja na kwamba ni mjamzito, atashiriki kama kawaida katika tamasha hilo.
"Wale ambao wanadhani kwamba mimba inaweza kunikwamisha, waje washuhudie jinsi nitakavyofanya kazi," alisema Nandy.