Kupitia video ya dakika mbili aliyoiposti katika ukurasa wake wa Instagram ikionesha mambo mbalimbali aliyoyapitia wakati akiwa chini ya lebo ya WCB kwa takribani miaka sita, Rayvanny amesema anaishukuru lebo hiyo ambayo imemfanya amekuwa msanii mkubwa ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake aliyekuwa Bosi wake Naseeb Nyange maarufu kama Diamond ameonesha kutokuwa na kinyongo na kutoa baraka zote kwa Rayvanny kwa kutoa maoni yake chini ya video hiyo na kuandika “NEXT LEVEL PRESIDENT”.