Mzee Jumbe avunjika mguu akikimbizwa na Jogoo ndotoni

12Nov 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mzee Jumbe avunjika mguu akikimbizwa na Jogoo ndotoni

Mwanamziki mkongwe wa Bendi ya Talent, Hussein Jumbe amevunjika mguu wa kulia baada ya kupiga ukuta akiwa ndotoni baada ya kuota anakimbizwa na kuku.

Hussein Jumbe.

Akiongea na kituo cha Televisheni cha ITV Tanzania jana, Jumbe amesema akiwa ndotoni alikuwa akiota anapigana na kuku na wakati akijaribu kumpiga akajikuta napiga ukuta.

"Kubwa ni hilo, inaonesha kuwa nimepiga kitu kizito na nimepiga kwa kutumia nguvu sana, kwahiyo nikiwa ndotoni nilikuwa naota ninapigana na kuku, Jogoo anataka kunidonyoa na mimi nataka nimpige hivi kumbe ndio napiga ukuta," alisema Jumbe na kuongeza kuwa;

Alisema kuwa ndoto hiyo sio ya kawaida na kwamba yeye anamuachia Mungu kwani ndiye muweza wa yote.

Akizungumzia kuhusu bendi yake kufanya maonesho, alisema kuwa bendi yake bado inaendelea na kwamba anatarajia siku ya Alhamis kuanza kufanya kazi. 

Jumbe ambae aliwahi kutamba na wimbo wake wa "Nachechemea" uliojizolea umaarufu mkubwa.