Mujungu amesema hayo leo Oktoba 02,2020 wakati wa ufunguzi wa kongamano la vikundi vya sanaa vinavyoelimisha jamii kuhusu sheria ya maadili ya viongozi wa umma na mgongano wa maslahi kupitia sanaa uliofanyika katika ukumbi wa Mlashi Mjini Bariadi.
Amesema wasanii wanapaswa kuwa wabunifu zaidi na waadilifu katika kutumia sanaa zao katika kuelimisha jamii kuhusu suala la maadili na athari zake.
Nae Kaimu Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi (Tabora), Gerald Mwaitebele amesema wameamua kutoa elimu kwa vikundi mbalimbali vya sanaa ili viweze kuelimisha jamii kupitia sanaa zao kuhusu sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.
Amesema lengo la kongamano hilo kwa vikundi hivyo vya wasanii ni kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wanajamii na kutambua mchango wao mkubwa katika kukuza na kusimamia maadili nchini.
Ameongeza kuwa wasanii wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali na ni vema sasa wakajikita katika uelimishaji wa elimu hiyo ya viongozi wa umma na mgongano wa maslahi kwa viongozi ili jamii na yenyewe iweze kutambua masuala hayo.
Nao baadhi ya wasanii waliohudhuria kongamano hilo wameahidi kuwa wawakilishi wa ofisi ya sekretarieti ya maadili ya umma kwa kutunga nyimbo mbalimbali zinazohusu maadili.










