TID amesema ameumizwa sana na kitendo hicho kwa sababu amekuwa akitumia akili yake na ubunifu wa kufikiria wazo la msemo huo, hivyo anaona kama anadhulumiwa na kutaka haki itendeke juu ya suala hilo.
“Nimehuzinuka sana na nimeona kwenye mitandao ya kijamii kuwa msemo wangu, ushairi wangu na ubunifu wangu unatumika kwenye kampeni za kisiasa bila ya kuwa na mawasiliano yoyote, nataka niseme kitu kimoja ni muda sasa wa usanii wetu utumike kwa usawa, nimehangaika kutumia akili yangu na nguvu ili kuutangaza huu msemo, naomba mnisaidie nimechoka kudhulumiwa” amesema TID.
Baada ya kusema hivyo TID amewa-tag Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Mwana Fa , na Cosota chombo ambacho kinasimamia haki miliki za wasanii.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu wamempitisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu kuwa mgombea wa nafasi ya urais Tanzania Bara. Wakati wa mchakato wa kura ya maoni ndani ya chama hicho yalionekana mabango yenye picha ya mgombea huyo wa urais yakiwa na kauli ya #Niyeye2020.