Ndoa hiyo kati yake na mumewe Duwa Msafiri imefungwa kisiri Novemba 20, mwaka huu nyumbani kwao Mlanzidi mkoa wa Pwani.
Akizungumza na EATV , Asha Boko amesema hakutaka ndoa yake ijulikane kwa sababu watu wangeweza kutia vizuizi.
"Ni kweli nimeolewa leo nyumbani kwetu Mlandizi, mume wangu anaitwa Duwa Msafiri na kesho kutakuwa na sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo, nilikuwa sijatangaza kwa sababu nisingeolewa watu wangenitangaza ila taarifa nimetoa kwenye familia, ndugu, jamaa na marafiki, mume wangu sio mtu maarufu hawawezi kumuiba kwa sababu anajielewa" amesema Asha Boko.
Asha Boko amefunga ndoa hiyo ikiwa ni mara yake ya pili baada ya mume wake wa kwanza kufariki dunia baada ya kushambuliwa na majambazi mwaka 2010.