Marioo alamba dili jipya Parimatch

03Nov 2022
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Marioo alamba dili jipya Parimatch

KAMPUNI ya Mchezo wa ubashiri ya Parimatch imemtangaza Msanii wa Bongo fleva Omary Ally  (Marioo) kuwa balozi wa kampuni hiyo ili kuwakutanisha mashabiki wake katika michezo ya ubashiri.

Akizungumza leo Novemba 03 Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Parimatch,Erick  Gerald amesema ujio wa Marioo umekuwa mzuri kwani kwa sasa Parimatch ndio kampuni inayoongoza kwa ubashiri ikiwa na ofa za kijanja na tovuti yenye muonekano mzuri,kasi kubwa.

"Ujio wa Marioo kwetu umekuwa mzuri kwani kwa sasa Parimatch ndio kampuni namba moja ya kubashiri ikiwa na ofa za kijanja na tovuti yenye muonekano mzuri, kasi kubwa huku ikiwa inatumia uwezo mdogo wa intaneti na kama hiyo haitoshi pia wateja wetu wataweza kushea mikeka yao kwa marafiki ili nao waweze kupata burudani kutoka Parimatch.," amesema na kuongeza kuwa;

“Tumechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Marioo kama balozi wetu kwa ajili ya kuzidi kupata burudani, yeye ni mtu ambaye amepambana na ameweza, Ila kikubwa ni kwamba huwezi ongelea burudani Tanzania bila ya kuacha kumtaja Marioo”.

"Kupitia Balozi wetu tuna hakika ataipeperusha vyema Chapa ya Parimatch kila eneo pamoja na kusaidia kutoa uelewa kwa wachezaji maana hasa ya kubeti ili wote tuweze kufurahi na kucheza kistaarabu.

Pamoja na hayo, kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia tumewaandalia ofa kabambe kwa wateja wetu pamoja na wadau wote wa michezo ya kubashiri ambapo kwa kushiriki katika promosheni hizo, kutamfanya mchezaji ajishindie zawadi nono ambazo zitamfanya ajihisi kama yupo Qatar." 

Kwa kumalizia niwakumbushe watanzania pamoja na wadau wote wa kubeti kuwa Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual.

Mbali na soka, kampuni pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match. Na zaidi ya yote kuna ofa kubwa ya bonasi ya 100% mpaka Sh. 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nasi!