Diamond Platnumz apata dili kuwa balozi wa vitenge vya Wax

19Sep 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Diamond Platnumz apata dili kuwa balozi wa vitenge vya Wax

Watengenzaje na wasambazaji wa kimataifa wavitambaa na vitenge vya Wax, HOLLANTEX, wamemtangaza msanii wa Muziki wa Bongo flava Diamond Platinumz kuwa Balozi mpya wa chapa ya bidhaa zao nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na HOLLANTEX, ubalozi huo kwa  na msanii huyo mwenye umri wa miaka 32, umemfikia kutokana na mtindo wake wa kucheza jukwani akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni yenye rangi tofauti hali ambayo inawavutia watazamaji wake sio tu kucheza muziki wake bali pia kupenda mavazi yake, ya nguo za vitenge zenye rangi bora za kitamaduni na za kuvutia.

Katika makubaliano ya ubalozi wake mpya, Diamond Platnumz atatumia kazi zake za kisanii kunadi rangi bora za bidhaa zitolewazo na kampuni ya Hollantex, zenye muundo  na ubora wa  hali ya juu ambazo zinalenga kutatua uhaba wa muda mrefu wa mavazi ya kitamaduni ya ubora wa vitenge vya Wax katika  soko la Tanzania na barani Afrika kwa Ujumla.

"Kwa kupitia ubalozi wa Diamond katika bidhaa hizi ni wakati muafaka sasa kwamba watu   nchini Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki sasa wanaweza kujua uwepo wa vitenge na vitambaa bora vya Wax sokoni vya chaguo lao," taarifa hiyo inamnukuu mwanzilishi wake, Thomas Fournier akisema.

 

Hollantex huzalisha na kusambaza vitambaa na vitenge vya wax vyenye rangi maridadi zaidi   vilivyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu sana. Kauli mbia ya bidhaa za  kampuni hii ni "Rangi yako, maisha yako,". 

 

Hollantex pia imejikita zaidi katika ubunifu, utengenezaji, na uuzaji wa vitambaa na vitenge bora vya wax vyenye kubeba historia ya Kiafrika na mitindo ya Magharibi na daima ni ubunifu katika suala la utaalamu wa rangi nzuri "kuvutia zaidi wateja wake na kuhakikisha juu ya uwepo wa bidhaa za Hollantex nchini Tanzania  ambo utatengeneza fursa za Biashara kupitia soko la mavazi kwa watanzania ili kuinua uchumi wa nchi,”

 

Taarifa ya kampuni inasemaKampuni hiyo ilitangaza kwamba hatua hiyo ilifikiwa baada ya mtaalamu wa sayansi ya rangi za mavazi Thomas Fournier, kutembelea sehemu mbalimbali za Afrika na kukutana na uzuri wa bidhaa za vitambaa vya Wax ambazo huchanganywa kwa uangalifunwa rangi na michoro ili kuonyesha tamaduni nzuri zaidi kwa wakazi wa bara hilo.

 

Fournier anasema kuwa katika ziara yake hiyo. aligundua kwamba uwepo vitambaa na vitenge vya Wax bora masokoni havikuwa vya kutosha kukata kiu ya wateja katika masoko mbalimbali.

“Kwa hiyo ubalozi huu wa Diamond unalenga kuwajulisha wafuasi wa mziki wake kuwa sasa bidhaa hizo ziko sokoni ni wakati Kiafrika kukutana na rangi hizo kuvutia, na hivyo basi, kila mtu anaweza kuvaa kitambaa chake bora cha kitenge cha Wax, afurahie kila siku ya maisha yake ya kupendeza.

Mbali na kuwa na uwepo na kufanya mauzo nchini Tanzania, kampuni hiyo pia inauza bidhaa katika nchi nyingine za kiafrika kama vila, Ivory Cost, Nigeria, Ghana, Togo, Benin, Niger, Mali, Guinée na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi nyingine nyingi barani Afrika. 

Diamond anaungana na wasanii wengine maarufa wa kiafrica e ambao pia ni Mabalozi wa bidha za Hollantex; kama vile Yemi Alade, Fally Ipupa, Sidiki Diabate; Toke Makinwa na Nancy Isime ambao wamekuwa sehemu ya timu ya Hollandex kwa miezi kadhaa katika kunadi vitenge hivyo beye rangi murua vya ubora wa daraja la juu katika ubora.