Alisema kuwa jina lake kwenye uigizaji limeshakuwa kubwa, hivyo ni muhimu awe makini na kazi anazoshirikishwa ili asijikute anashindwa kufikia malengo aliyojiwekea ya kuwa msanii wa kimataifa.
"Jina langu limekuwa kubwa na hasa baada ya kupata tuzo kule Nigeria hivyo ni muhimu niwe makini ninapoombwa kushirikishwa katika filamu nisije kukubali hata zile ambazo zinashusha hadhi yangu," alisema.
Lulu ambaye sasa ana filamu mpya iitwayo 'Ni Noma', aliongeza kuwa wapo baadhi ya wasanii, ambao wanadhani kwamba kushiriki filamu nyingi ndiyo kupata umaarufu, lakini kwake hilo halipo kabisa kwa vile anajitambua na kujithamini.









