Ombi hilo limetolewa na msanii nyota, Hisany Muya ‘Tino’, alipokuwa akizungumza jinsi anavyoliona soko la filamu jinsi lilivyo kwa sasa na hatima yake.
Alisema kuwa filamu za nje zinaua soko la ndani na kusababisha wasanii kuishi kwa shida kwa vile hata wakiandaa kazi zenye ubora kiasi gani zinakosa soko la uhakika.
"Tunaomba serikali itusaidie kwa hili kwani filamu kutoka nje ni tatizo, zinaua soko letu, hazilipi ushuru zimezagaa kila kona huku zikiuzwa kwa bei ya kutupwa," aliongeza Tino kuhusu filamu hizo zinazouzwa hadi kwa Sh. 1,000.










